Michezo

Rooney aomba Mapumziko

 

Mshambuliaji wa Man United na England Wayne Rooney ametaka kuwepo kwa mapumziko ya ligi kuu ya England wakati wa majira ya baridi ili kuipa nafasi timu ya taifa kujiandaa na michuano mbalimbali.

Tamko la Rooney linakuja kutokana na mfumo wa ligi wa England ambao unatofautiana na za nchi nyingine za Ulaya zikiwemo Hispania,Italia,Ufaransa na Ujerumani ambazo zimekuwa na jadi ya mapumziko wakati wa majira ya baridi mwishoni mwa mwaka.

England imeshindwa kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa tangu mwaka 1990 iliposhiriki michuano ya kombe la Dunia na kufika nusu fainali. Rooney ambaye anaandamwa na vyombo vya habari kutokana na kushuka kwa kiwango chake hivi karibuni amesema anaamini kuwamba kuwa na mapumziko itakua ninafasi nzuri kwa taifa hilo.

Mapumziko ya ligi yataisaidia timu ya England na pia vilabu. Kuelekea mwishoni mwa mwaka kuna mechi nyingi zinazosogezwa mbele kutokana na mvua na barafu. Huwa ni jambo la busara kuwa na mapumziko.

‘Ni nafasi nzuri kwa washambuliaji pindi wanapokutana na mechi ngumu za mfululizo, hasa katika nchi yetu ambapo mchezo ni wa nguvu na kasi,’ alisema Rooney.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents