Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Rooney aifikia rekodi ya Sir Bobby Charlton

By  | 

Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa Uingereza, ameifikia idadi ya mabao ya Sir Bobby Charlton ambaye aliweka rekodi ya kufunga idadi kubwa zaidi ya mabao akichezea klabu ya Manchester United.

Rooney ambaye saivi ana miaka 31, alifunga bao wakati wa mchuano kati ya Manchester United na Reading na kufikisha jumla ya mabao 249 kwa mechi 543.

Rekodi hiyo ya Charlton imekuwepo tangu mwaka 1973.

Mwaka 2015 Rooney alivunja rekodi ya Charlton ya mabao 49 aliyofungia timu ya taifa ya Uingereza na kuongeza idadi hiyo hadi mabao 53.

Rooney ambaye alihamia Manchester United mwaka 2004 akitokea Everton kwa kitita cha pauni milioni 27 mwaka 2004, na bao lake la kwanza alifunga dhidi ya Fenerbahce.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW