Burudani

Roma Mkatoliki kuachia ngoma mpya kwenye Serengeti Fiesta Tanga

Roma Mkatoliki ametangaza rasmi kuachia ngoma zake mpya usiku wa Serengeti Fiesta-Tanga, katika uwanja wa Mkwakwani Jumamosi hii.

roma

Roma ambaye ni mzaliwa wa Tanga na kipenzi cha wengi jijini humo amesema ngoma hizo mpya zitasindikizwa na vibao kama vile Mr. President, Pastor, Mathematics, 2013, KKK pamoja na ngoma mbalimbali alizoshirikishwa na wasanii mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Kauli mbiu ya Serengeti Fiesta mwaka huu ni “Sambaza upendo,”

Roma ambaye kwa sasa ni kati ya wanamuziki wakubwa hapa nchini, amekuwa akishiriki Serengeti Fiesta tangu mwaka 2007. “Serengeti Fiesta imenikuza kumuziki…nimeanza kupanda katika majukwaa ya Serengeti fiesta miaka saba iliyopita na katika kipindi chote hicho nimekuwa nikipata ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa mashabiki zangu na nnamshukuru Mungu kwamba sijawahi waangusha mashabiki zangu,” alisema Roma.

Roma ameishukuru Serengeti Fiesta kwa kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka pande zote hapa nchini. “Kupitia Serengeti fiesta, imekuwa rahisi sana kwa wasanii kubadirishana mawazo…kukutana na mashabiki zetu na vile vile kipata fursa mbalimbali ambazo si rahisi kuzipata tukiwa mtaani.”

Roma amewaasa wasanii na wadau wa muziki kutumia fursa vizuri fursa zinazoambatana na Serengeti fiesta ili kujinufaisha kimuziki na katika maisha yao ya kawaida. Wasanii wengine watakao lipamba jukwaa la Serengeti Fiesta Tanga ni pamoja Recho, Chege and temba, Alikiba, Ney wa mitego, Stamina, Jux, Linah, Vanessa mdee, Mr Blue, Mkubwa na wanae, Ommy Dimpoz, Barnaba, Young Killer na Madee.

Waandaaji wa tamasha hili wamewahakikishia Wanatanga usalama wa hali ya juu na kusema kwamba serikali ya Jiji la Mwanza iko makini na itatoa ulinzi tangu mwanzo wa tamasha mpaka mwisho.

Baada ya Tanga, burudani hili la nguvu litashuka katika mikoa mbalimbali kama Mara, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Moshi, Arusha, Mtwara na na hatimaye jijini Dar es Salaam ifikapo Oktoba 18 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents