Burudani

Roma: Kushangiliwa sana jukwaani na mashabiki ndio msanii umefanya show kali na nzuri? Swali kwa mashabiki

Roma ni rapper mwenye mashabiki wengi Tanzania, lakini hilo halijamzuia kuhoji mashabiki wake swali ambalo kwa upande mwingine linaweza kusaidia na wasanii wengine.

Roma2

Kupitia ukurasa wake wa Facebook rapper huyo wa ‘2030’ amewauliza mashabiki wake ni kitu gani ambacho hupelekea msanii kufanya show nzuri jukwaani ukiachilia shangwe za mashabiki ambazo zinaweza kuchangiwa na vitu vingi hta kama show ya msanii si nzuri.
Roma3
Hiki ndicho Roma ameandika, na mwishoni unaweza kutoa comment yako kujibu kile alichouliza.

Juzi tulilijadili hili na wasanii wenzangu,hatukupata ‪#‎muafaka‬ sasa nalileta kwenu!!
Haimuhusu mtu ila tunajadili maendeleo ya muziki wetu!!!

ETI KUFANYA SHOW NZURI NA KALI NDIYO KUKOJE????
MSANII HADI AFANYAJE KWENYE SHOW NDIO MNASEMA AMEFANYA SHOW KALI NA AMETISHA???
Nijibuni ninyi mashabiki!!!?

Mfano!!!
Kushangiliwa saaaana jukwaani na mashabiki ndio umefanya show kali na nzuri?

Kuna siku ‪#‎cocobeach‬ ‪#‎bibicheka‬ alipanda akashangiliwa saaanaaa na maraia!!! Japo anaimbia ‪#‎play_back‬ na kuna muda haimbi kabisaaa… Yani alishangiliwa mno kuliko msanii ‪#‎flani‬ mkubwa sana alipopanda!!

Nikajiuliza hivi ‪#‎bibi‬ ndio amepiga show kali na kafunika!!?? Kuliko huyu flani!!?
Nakosaga majibu!!

Kuna artist wanafanya ‪#‎playback‬ ktk show kila mwaka na kuna muda hawaimbi wanadanganya tu wameshika ‪#‎mic‬ kumbe cd ndio inaimba!! Lakini kesho naambiwa jamaa wamefanya sana show kali!!wameua!!!

Kuna mwaka flani tulipiga show ‪#‎Tanga‬ mimi na ‪#‎jos‬ mtambo na ‪#‎jcb‬ basi kila aliepanda aisee mashabiki walimtazama tu bila kushangilia!! Wakajua nikipanda mimi kwakuwa ni kwetu ndio nitaamsha…doooh kupanda mimi ndio kabisaaaa ziiiii raia wananishangaa tu!! heri hata kina #jcb….eti baada ya sisi kumaliza wakapandishwa jamaa wawili washindane kunywa ‪#‎soda‬ nani atawahi kumaliza….hahahahahah acha watu waanze kuwashangilia aisee…hahahahaj nilishangaa sana!! Sasa apo sisi na jamaa nani kafanya show kali??

Usiku wa matumaini juzi uwanja wa ‪#‎taifa‬ yule mnigeria ‪#‎yemi_alade‬ honest.. alizingua big tym kuliko wabongo wote waliopanda nae….heeeee kesho naona ‪#‎magazeti‬ yameandika
‪#‎YEMIALADE‬ AFUNIKA DAR……ahhahhaaha Nikasema labda mm ndio sikumuelewa!!!

Kuna wengine jukwaani wanadance na kujituma saaana lakini hawashangiliwi…aaaf wengine wakipanda wanavua nguo jukwaani na kucheza nusu utupu hawaimbi wala nn…mic ipo chini huku anachezesha mdomo tu na kukatika nusu utupu watu wanashangilia!!
Hawa nao ndio wanafanya show kaliiii???
JE KUPI NDIO KUFANYA SHOW KALI NA KUFUNIKA???

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents