Burudani

Roma azungumzia video ya Maumivu na kwanini hatoutumbuiza wimbo huo kwenye show zao

Rapper Roma Mkatoliki, amewatataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya video ya wimbo ‘Maumivu’ aliofanya na Bob Junior.

IMG-20140809-WA0011_full

Akizungumza na Bongo5 leo, akiwa safarini kuelekea mjini Musoma kwenye Serengeti Fiesta 2014, Roma amesema yeye na Bob Junior wamekubaliana kutouimba wimbo huo kwenye show zao.

“Tupo speed sana kwenye maandalizi ya video tupo kwenye tour, Bob ana ziara na mimi kama unavyoniona. Sasa hivi tupo mbioni kufanya video ambayo itachukua kama wiki mbili mpaka kukamilika na kuweza kutoka,” amesema Roma.

“Halafu ndo inakuwa full package ya nyimbo kwamba audio ilishatoka pamoja na video. Kutokana na tour ambazo tunazifanya kuna kitu ambacho tumejiwekea mimi na Bob Junior, kwamba hatakiwi kuiperform ile nyimbo kwa sasa na Roma pia hatakiwi kuiperform hiyo nyimbo kwa sasa. Halafu itafikia time tutaanza kuiperform kwa sababu kuna tour zimetuingilia katikati wakati na sisi tunarelease ngoma ikasababisha tutofautiane muda wa kuperform hiyo nyimbo.”

“Hiyo inatusaidia kwa sababu inawapa watu kiu, watu wakiona Roma yupo kwenye Fiesta wanategemea Roma ataimba wimbo wa Maumivu Halafu sasa Roma anakuwa haimbi, halafu itafika time tutaanza kufanya tour kwa sababu ya wimbo Maumivu na tunaamini itafanikiwa baada ya muda fulani,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents