Burudani

Roma atimiza ahadi ya kufanya wimbo Sharobaro Rec, wimbo unaitwa ‘Maumivu’

Hitmaker wa Mathematics Roma Mkatoliki ametmiza ahadi yake ya kwenda kufanya wimbo katika studio za Sharobaro Records chini ya producer Bob Junior aliyoweka wakati wa kombe la dunia kama Brazil ingefungwa na Ujerumani. Katika studio hiyo, Roma amerekodi wimbo uitwao ‘Maumivu’.

1661859_10152437223664962_6158055271820031636_n
Roma na producer Bob Junior wakiwa studio

Akizungumza na Bongo5 leo, Bob Junior amesema amefurahishwa na uamuzi wa Roma wa kumuamini na kuanza kufanya kazi hiyo ambayo itatoka wiki ijayo.

“Roma jana alikuwa kwangu na tumeandaa ngoma mpya inaitwa Maumivu na itatoka next week,” amesema Bob Junior. “Nashukuru ameweza kuelewa kuwa nina kitu gani, kaja hapa hakuamini alichokisikia kwa sababu nilimwambia nafanya Hip Hop nzuri sana lakini hakuniamini lakini jana kaja nafikiri alifika saa 4 akaondoka saa kumi asubuhi, yaani saa kumi alfajiri. Tumefanya kazi tumeishia nusu lakini tutaimalizia leo, lakini next week itatoka hii collaboration.”

10502042_10152437223614962_7652574042397661009_n
Huu ndio ujumbe wa Roma uliokuwa na ahadi hiyo

We Did 2Day..Roma & Mi Bob Junior…Unafikiri itakuwaje ikotoka? Ahadi Yake imetimia Am Happy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents