Burudani

Roma aitaja sababu ya hip hop ya Bongo kutohusishwa kwenye tuzo za kimataifa (Video)

Hivi karibuni tuzo za Afrimma zilitangaza majina ya wasanii watakaowania mwaka huu. Tofauti na miwili iliyopita, mwaka huu wasanii wengi zaidi wa Tanzania wametajwa kuwania, lakini hakuna hata mmoja wa hip hop aliyetajwa.

Roma2

Niliamua kumuuliza rapper Roma kwanini anadhani hip hop ya Bongo imeendelea kutotambulika kwenye tuzo za kimataifa licha ya kuwa na wasanii kama Joh Makini, Fid Q, Mwana FA na wengine walioshuti video zenye viwango na zingine kushika chati za MTV na Trace.

Mfano ni jinsi ambavyo nyimbo za Joh Makini ‘Nusu Nusu’ na ‘Don’t Bother’ aliyomshirikisha AKA wa Afrika Kusini zilivyofanya vizuri. Roma amesema kama zilivyo tuzo za Tanzania, hata zile za nje zimekuwa na figisu figisu na kubaniwa kwa baadhi ya wasanii.

Kingine amedai kuwa kupigwa kwa video nje ya nchi sio kigezo tosha na kwamba kuna mengine yanahitajika ikiwemo rappers wa Tanzania kuanza kufanya show nje ya nchi.

Amedai kuwa wasanii wengi wa Nigeria wametengeneza sifa ya kuweza kujitanua na kuja hata katika nchi za Afrika Mashariki na kufanya show huku wakilipwa fedha nyingi.

“It’s okay kazi yako inaenda, huenda audio au video inapigwa na inakaa katika chati sio kigezo tosha, unaweza kwenda pale Nigeria stadium ukaijaza, wakakupokea hadi wakasema ‘this guy is from East Africa na ni noma’,” amesema Roma.

Roma amedai kuwa huo ni mwanzo wa hip hop ya Tanzania kufanya vizuri hivyo harakati zinazofanywa na rappers ziendelee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents