Michezo

Roger Federer ajitoa katika mshindano ya wazi ya Ufaransa

Roger Federer amejitoa katika mshindano ya wazi ya Ufaransa mwaka huu baada ya kushindwa kupona maumivu ya mgongo yanayomkabili.

roger-federer-070915-getty-ftrjpg_rduhtoxzytug1ac4wdn8cvjxv

Federer mwenye miaka 34 hakuweza pia kucheza katika michuano ya wazi ya Madrid mapema mwezi huu.

Alirejea katika mashindano ya wazi ya Italia lakini aliondolewa kwenye raundi ya tatu na Dominic Thiem.

”Ninaendelea vizuri lakini sio kwa asilimia 100,”alisema mchezaji huyo namba tatu kwa viwango vya mchezo huo duniani. ”Nafikiri naweza kujiweka pabaya kama nitacheza katika mashindano yoyote bila kupona vizuri”. ”Maamuzi haya hayakuwa mepesi kufanya,lakini niliamua kuacha kucheza ili pia nipumzike vyema”

Hii inamaanisha kuwa Federer atakosa kucheza Grand Slam kwa mara ya kwanza ndani ya karne hii.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents