Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Roc Nation Sports ya Jay Z yamnyatia kinda wa Man United

By  | 

Bosi wa lebo ya Roc Nation, Jay Z ambaye pia anamiliki kampuni ya uwakala wa wachezaji inayojulikana kama Roc Nation Sports anadaiwa kumnyatia mchezaji kinda wa Manchester United ambaye anachezea kwenye kikosi B cha timu hicho Roshaun Williams.

Kwa sasa Roshaun ana miaka 18 na anasimamiwa na baba yake mzazi. Japo anacheza kwenye kikosi cha pili cha Manchester United lakini pia mara nyingi hufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun, mawakala wengi wamekuwa wakivutiwa kumsajili mchezaji huyo ambaye anaonekana kuja kufanya vizuri sana hapo baadaye.

“Everyone’s trying to sign Roshaun because he looks like he is going to be the next big talent for England. The move from Jay Z has got all the football world talking because it’s a big statement of how he sees his company’s future. He has a big role in the company and football is an obvious market for him to get into with his sports business,” kimesema chanzo hiko.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW