Promotion

Road To MAMA 2010..noma!!

Road to MAMAs 2010

 

Sherehe za awali ambazo huandaliwa na kituo cha televisheni cha MTV Base Road To MAMA zinatarajiwa kuwa baab kubwa, zaidi ya wasanii wanne wa kimataifa wanatarajiwa kutua bongo kupiga shoo katika wiki ya pili ya mwezi wa kumi na moja.

Jumla ya wasanii watatu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati wameshathibitishwa kuporomosha burudani ya ukweli akiwemo msanii kutoka Congo Fally Ipupa, Amani kutoka Kenya na Joh Makini, wakisindikizwa na wasanii wawili kutoka marekani na mmoja kutoka Jamaica.

Hii inazidi kuifanya Tanzania nchi yenye bahati zaidi kiburudani kwa mwaka huu kwani tayari wasanii kadhaa wameshatinga bongo tangu kuanza kwa mwaka huu.

Shoo hiyo itakuwa ikihusiana na shughuli ya mpira wa miguu ambapo timu kadhaa za ulaya kutoka ujerumani na ufaransa zinatarajiwa kuja Tanzania kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa timu ya African Lyon kwa wamiliki wapya amabo nio watanzania na wamarekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents