Habari

Ripoti: Wanaume wa Afrika Kusini waongoza duniani kwa kufanya mapenzi mara chache zaidi

Imebainika kuwa wanaume wa Afrika Kusini hufanya mapenzi nusu ya wanaume wengine duniani, kwa mujibu wa survey iliyofanyika na kutangazwa Jumanne hii nchini humo.

Sexless-Marriage

Kwa mujibu wa survey iliyofanywa na kampuni ya madawa ya Pharma Dynamics, wanaume nchini humo hufanya mapenzi kwa takriban mara 52 tu kwa mwaka. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume wengine duniani hufanya mapenzi 104 kwa mwaka (average).

Zaidi ya wanaume 500 wenye umri kati ya miaka 18 na 55, waliopo kwenye mahusiano ya muda mrefu (committed relationship), walishiriki kwenye survey ya nchi nzima ya kampuni hiyo ya madawa. Asilimia 22 ya wanaume wa nchini humo walibainika kufanya mapenzi mara tatu kwa mwezi, wakati asilimia 16 wakiwa kwenye uhusiano usiokuwa na ufanyaji mapenzi kabisa (sexless relationship).

Msemaji wa kampuni hiyo, Mariska van Aswegen alisema wanaume walitupia lawama uchumi, presha za kazi, na usumbufu kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii kama sababu za kutofanya mapenzi kwa wingi. Asilimia 23 ya wanaume walioshiriki kwenye zoezi hilo walikiri kupatwa na hali ambayo viungo vyao vya uzazi hushindwa kusimama kwaajili ya tendo hilo ambalo kitaalam hujulikana kama ‘erectile dysfunction’ (ED), na asilimia 12 kati yao wakisema wamekuwa na tatizo hilo kwa miaka kadhaa.

Van Aswegen amedai kuwa ED huwaathiri asilimia 40 ya wanaume wa Afrika Kusini.

“Walipoulizwa ni mara ngapi madaktari wa Afrika Kusini hutibu ED katika shughuli zao, asilimia 80 kati yao walisema zaidi ya mara 10 kwa mwezi – ongezeko kubwa katika kipindi cha miaka michache,” alisema.

Katika utafiti huo, ilibainika kuwa asilimia saba ya wanaume walitumia dawa za ED ili kuongeza uwezo wao katika tendo hilo, japokuwa hawakuwa wakizihitaji. Van Aswegen alidai kuwa hiyo ni hatari kwakuwa wanaume hao wanaweza kujikuta wakitegemea zaidi dawa hizo na hivyo kuwafanya wawe na matatizo ya ED.

Alisema kuwa ni vijana wenye umri mdogo ndio waliobainika kupenda kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.

Kwa mujibu wa survey, hiyo, teknolojia za kisasa ndizo zimepelekea kushuka kwa ufanisi wa wanaume katika mapenzi ambapo tabia ya kulala na simu au tablets ikidaiwa kuwa chanzo. “Siku hizi watu wanazishika smartphones kuliko wanavyowashika wenza wao,” alisema Van Aswegen. “Ukweli kwamba kazi huja katika nyumba zetu sasa hufifisha mstari kati ya kitanda na ulimwengu wa nje.”

Chanzo: TimesLive.co.za

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents