Burudani

Ripoti: Kanye West aanza kutengeneza muziki mpya akiendelea na matibabu

Ni ngumu kumtenganisha Kanye West na muziki. Kwa mujibu wa ripoti ya TMZ, rapper huyo ameanza kupika kazi mpya wakati akiendelea na matibabu.

kanye-wang

Mtandao huo umedai kuwa ameshaanza maandalizi ya album yake mpya.
Vyanzo vimedai kuwa tangu arejee nyumbani amekuwa mtulivu na makini zaidi katika mambo yake.

Vimesema ametengeneza studio ya muda kwenye jumba lake la kifahari la Bel-Air ili awe na muda wa faragha anaohitaji ili apone kabisa wakati pia akitengeneza muziki mpya.

Vimesema kuwa Kanye anafananisha kilichomtokea kama ajali mbaya aliyowahi kuipata pamoja na kifo cha mama yake. Vimsema anajisikia kutengeneza nyimbo kama zile zake bora zikiwemo “Through The Wire” na ‘808s’ baada ya masahibu hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents