Michezo

Rio Ferdinand afunguka alivyoumizwa na kifo cha mkewe

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand amefunguka kwa kueleza kuhusiana na kifo cha mkewe. Ferdinand amesema aliumia na kuteseka sana kutokana na kifo hicho kwa kuwa hakuwa amejiandaa.

Rebecca alifariki dunia Mei, 2015 baada ya kuugua ugonjwa wa kansa ya ziwa kwa kipindi kifupi tu.
Mauti yalimkuta Rebecca ambaye alimuacha Rio na kazi ya kulea watoto wao watatu na Rio amesema hakuwa amejiandaa kwa kuwa hakujua masuala ya malezi ya watoto.

Rebecca ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 34 na kuwaacha watoto wake watatu mkubwa akiwa na umri wa miaka 10, miaka nane na wa mwisho mwenye miaka mitano.

“Nilipata matatizo mengi sana kwa kuwa siku nimejiandaa, sikutegemea kama hali hiyo ingetokea katika kipindi kile.

“Sikujua mambo ya kubembeleza watoto kama ilivyotakiwa, lakini sikuwa na namna,” alisema Rio mwenye umri wa miaka 38.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents