Burudani

Rihanna na Kim Kardashian waongoza mastaa wengine kupinga sera za Trump

Hiki ni kipindi ambacho Rais wa Marekani Donald Trump hatakuja kukisahau katika maisha yake japo ameonekana kuziba masikio na kufanya kile ambacho anakiamini ni sahihi kwa upande wake. Mastaa wa nchi hiyo wakiongozwa na Rihanna wameendelea kuungana na wananchi wengine kupinga sera zake.

Rihanna na Kim Kardashian wameendelea kuwa upande wa wananchi tangu yalipofanyika maandamano ya Women’s March yaliyofanyika duniani kote wiki mbili zilizopita. Mastaa hao wa kike wenye nguvu kubwa katika tasnia ya burudani wameungana na mastaa wengine akiwemo Chris Brown, John Legend na French Montana kupinga maamuzi ya Rais huyo kuzuia waislamu kuingia nchini Marekani.

Kupitia mitandao ya kijamii mastaa hao wameonyesha kutoungana na Trump juu ya maamuzi hayo huku Rihanna akienda mbali zaidi kwa kumuita Rais huyo Nguruwe. “Disgusted! The news is devastating! America is being ruined right before our eyes! What an immoral pig you have to be to implement such BS!!,” ameandika Rihanna katika mtandao wa Twitter.

Naye Kim kupitia mtandao huo ameweka picha ya twakwimu inayoonyesha jumla ya watu wa Marekani waliouawa na magaidi ikiwa ni watu 9 huku idadi ya raia wa nchi hiyo waliouwana wenyewe kwa wenyewe ikiwa ni 11737.

Chris Brown kupitia mtandao wa Instagram, ameweka picha ya mwanamke aliyevaa hijabu huku akiwa amebeba bango lililoandikwa: Wearing a Hijab does not make me any less American than you.

Wakati huo huo rapper French Montana ambaye ana asili ya nchini Morocco, kupitia mtandao huo ameandika ujumbe mzito unaosomeka, “Love this ❗️More people with power need to stand up ❗️This how war start ❗️And innocent people suffer while you’re somewhere playing golf. This country belong to the Indians. We all immigrants❗️You can’t point fingers with a dirty hand❗️What do u expect people to do when u tell them they can’t see they family ???? u can’t kick the people that built this country out! ” immigrant “❗️I’m disgusted to the highest level!.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents