Burudani

Rihanna ajitengenezea rekodi nyingine Marekani

Juhudi huzaa matunda. Rihanna anazidi kutengenezea heshima na kujiwekea rekodi zake binafsi kupitia muziki wake.

Muimbaji huyo ametunukiwa tuzo ya Platinum na chama cha Recording Industry cha Marekani kupitia nyimbo zake mbili ‘Love on the Brain’ na ‘Sex With Me’ ambazo zinapatikana kwenye albamu yake ya ANTI huku wimbo wake wa ‘Work’ aliomshirikisha Drake ukipatiwa cheti cha 5X Platinum.

Baada ya kupatiwa heshima hiyo, lebo yake ya Roc Nation inayomilikiwa na rapper Jay Z ilimpongeza kupitia mtandao wa Twitter kwa kuandika, “Congrats @Rihanna! “Love On The Brain” & “Sex With Me” are certified Platinum and “WORK” ft. @Drake is certified 5X Platinum @RIAA!.”

Kwa sasa Rihanna ameonekana kujikita zaidi kwenye tasnia ya mitindo pamoja na kutetea haki za wanawake huku akionekana wiki iliyopita kwenye maandamano ya Women’s March yaliyofanyika mjini New York ya kupinga Urais wa Donald Trump.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents