Burudani

Rihanna aitukana TV ya CBS ‘f**k You’ baada ya kusitisha kutumia wimbo wake kwenye tangazo

Hatimaye Rihanna ameamua kufunguka yaliyomo moyoni baada ya kituo cha runinga cha Marekani cha CBS kutoa wimbo wake kwenye intro ya matangazo ya mechi za NFL kutokana na skendo ya mchezaji Ray Rice ya kumpiga mkewe.

Rihanna-Red-Lip-600-x-450

Kituo hicho cha runinga kilisitisha kutumia wimbo wa Rihanna kutokana na jinsi alivyojihusisha kwenye skendo hiyo.
CBS ilikuwa iendelee kuutumia wimbo huo hadi pale Rihanna, aliyekuwa mhanga wa ukatili wa nyumbani mwaka 2009 kutoka kwa mpenzi wake Chris Brown, kuwashutumu mabosi wa TV hiyo kwa kumuadhibu kwa kosa la mtu mwingine na kusisitiza kuwa hakutaka waucheze wimbo huo wiki hii.

Channel hiyo imedai kuwa kwa kutumia wimbo huo isingekuwa inatoa picha nzuri kwa skendo ya ukatili wa majumbani inayomkabili mchezaji wa Baltimore Ravens.

“CBS you pulled my song last week, now you wanna slide it back in this Thursday? NO, F— you! Y’all are sad for penalising me for this,” Rihanna alitweet.

Rihanna alitweet maneno hayo kwakuwa wiki iliyopita baada ya kusimamishwa kwa Rice, CBS iliuondoa ufunguzi (uliokuwa na wimbo wa Rihanna) wenye wimbo huo kwaajili ya matangazo ya mechi za NFL na kuweka breaking news ya hatua hiyo na maoni kuhusu ukatili wa MAJUMBANI.

Kutokana na Rihanna kuchukia kukatwa kwa wimbo huo, kituo hicho sasa kimedai kuwa kimeamua kuutoa kabisa wimbo huo kwenye intro hiyo.

“Beginning this Thursday, we will be moving in a different direction with some elements of our Thursday Night Football open,” maelezo ya CBS Sports yamesema. “We will be using our newly created Thursday Night Football theme music to open our game broadcast.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents