Burudani

Rick Ross awadiss Birdman na Nicki Minaj kwenye album mpya

Usiku wa Alhamis, Rick Ross ameachia album yake mpya, ‘Rather You Than’ Me na tayari imetengeneza vichwa vya habari hususan baada ya kuwadiss watu wawili, Nicki Minaj na Birdman.

Kwenye wimbo wa kwanza kufungulia album ‘Apple of My Eye’ Ross anarap, “ told Meek I wouldn’t trust Nicki/Instead of beefing with your dog you just give him some distance,” akizungumzia kuvunjika kwa uhusiano wa Minaj na Meek Mill. Wiki moja iliyopita Mill alinukuu sehemu ya mistari hiyo na kuweka kwenye picha aliyopost Instagram akiwa na Ross, “Rozay been told me don’t trust you.”

Ross pia amemchana CEO wa Cash Money Records, Birdman kwenye wimbo ‘Idols Become Rivals.’Wimbo huo mzima umejaa mashairi ya Ross akilalamika jinsi Birdman alivyomuangusha.

Mashairi yaliyozusha mjadala zaidi ni kuhusu Lil Wayne ambaye amekuwa kwenye ugomvi na Birdman kwa miaka sasa.

“I pray you find the kindness in your heart for Wayne/His entire life, he gave you what there was to gain/I watched this whole debacle so I’m part to blame/Last request, can all producers please get paid,” anarap Ross kwenye verse ya pili.

Mapema jana, Ross aliweka post Instagram baada ya ‘Idols Become Rivals’ kuvuja.

Akiweka picha ya Lil Wayne, Rozay ameandika:

The Level of respect and Love that I have for WAYNE makes it hard to sit back and not speak on the situation.The streets need you.Being a Boss means having the courage to say the things everybody thinking but scared to say.I can’t wait for you to hear it.Midnight. #idolsbecomerivals

Baadaye Wayne aliscreenshot post hiyo na kuandika kwenye Twitter: dam big bro that msg hit me in the heart and put the motivation on automatik start. I needed that. 1 boss 2 another.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents