Pics: Rick Ross apagawa kusikia watu wakiimba nyimbo zake zote, mashabiki wamkubali

Ilikuwa ni mida ya nane na kama dakika 15 hivi za usiku baada ya list ndefu ya wasanii wa nyumbani kupiga show, pale mtu aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu kupanda kwenye stage ya Fiesta, Dar es Salaaam naye si mwingine bali ni Rick Ross.

Kabla ya kuingia, stage iligeuka kuwa eneo busy kwa muda baada ya watu walioambatana naye kuhakikisha usalama kwanza. Ile anaingia tu hivi, Dj aliyeambatana naye alisikika akisema ‘Tanzania mambo vp” kitendo kilichochochea shangwe refu kutoka kwa umati mkubwa uliokuwa umefurika Leaders Club.

Kukaribisha ujio wake kwenye stage, ilisikika ngoma maarufu aliyoshirikishwa na Meek Mill, ‘Imma Boss’ ambayo ilipopigwa tu hivi umati wote ulipagawa na kuanza kupiga makelele. Kelele hizo ziliambatana na fataki za kila aina na kutengeneza rangi nzuri kwenye anga la Leaders.

Kwa hakika Rick Ross hakuwa ametegemea mapokezi kama hayo kiasi cha kusikikia akisema mara nyingi jinsi anavyojisikia ‘I feel the love’. Kilichomshangaza zaidi ni jinsi watu walivyokuwa wakiimba nyimbo zake bila kukwama na kumfanya atabasamu mara nyingi. Kila alipoigeuza mic kwa mashabiki waitike mashairi yake, umati huo haukumwangusha kwani ulijibu kama alivyotaka.

Kilichofurahisha zaidi ni jinsi alivyokuwa akiconnect maongezi aliyokuwa akitoa na wimbo uliofuata. Kwa mfano kabla ya kuimba Hold Me Back alisikika akisema kuwa hakuna mtu anayeweza kukurudisha nyuma kama tu ukiajiamini na kile unachokifanya.

Nyimbo zilizowashika zaidi wapenzi wa ngoma zake ni pamoja na BMF, Aston Martin Music, Hustlin, I am not a star, Hold me back na Push.

Mara nyingi alikuwa akisikika akiwaambia mashabiki ‘Can I here Rozay’ huku DJ akichombeza na sauti maarufu ya msichana isemayo ‘Maybach Music’.

Hakusau kusifikia wasichana warembo wa Dar na kusema kuwa imemlazimu kukaa kwa siku moja zaidi ili apata fursa ya kuwashuhudia vizuri.

Mpaka anamaliza show yake, Rick Ross ameondoka na picha moja kuhusu Tanzania nayo ni kwamba ana mashabiki wake ni wengi mno na nchi hii watu wanaijua Hip Hop ya Marekani.

Tutegemee, Tanzania kuitaja kwenye mashairi yake yajayo. Ameipenda Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents