Burudani

Rick Ross aeleza jinsi alivyomvisha pete ‘kibabe’ mchumba wake bila kupiga goti

Wiki hii rapper Rick Ross alifanyiwa mahojiano na kipindi maarufu cha The Breakfast Club kupitia Power 105 na aliongozana na mchumba wake Lira Galore aliyemvisha pete hivi karibuni.

rozay na mchumba wake

Miongoni mwa mambo aliyoyagusia katika mahojiano hayo ni pamoja na kumchumbia Lira.

Rozay ambaye ni boss wa MMG aliweka wazi kuwa katika lile tendo la kumvisha pete ya uchumba mke wake mtarajiwa ambalo kwa wanaume wengine hunyenyekea kwa kupiga goti moja chini na kuuliza swali ‘will you marry me’, kwake ilienda tofauti.

Alipoulziwa alivyomchumbia Lira hiki ndicho alichokisema wakati wa kupropose;
“Here go the biggest ring in the store ya dig. Now lets go to Buddakan.” Alipoulizwa kama alipiga goti alijibu kuwa hawezi kupiga goti. “Nah, I ain’t get down on one knee,”.

Rozay aliongeza kuwa bado hawajapanga tarehe ya kufunga ndoa.

Tazama mahojiano hayo

https://youtu.be/KesGJBz6f3U?t=14m31s

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents