Burudani

Rich Mavoko ataja sababu zilizomfanya awe kimya kwa zaidi ya mwaka mmoja

Rich Mavoko ameachia wimbo mpya Jumanne (Nov.24), ikiwa ni mwaka mzima na miezi miwili toka alipoachia single ya mwisho ‘Pacha Wangu’.

mavoko new

Wakati akitambulisha single mpya iitwayo ‘Naimani’ kupitia XXL ya Clouds Fm, Mavoko amezitaja sababu zilizomfanya asitoe wimbo kwa kipindi kirefu toka mwaka jana.

“Cha kwanza Pacha Wangu ni wimbo nimetoa mwezi wa 9 (2014) lakini pia imekuwepo kwa muda mrefu, sisemi kwamba natakiwa nitoe nyimbo ikae muda mrefu hapana.”

Mavoko aliendelea,

“lakini kusuasua kwangu pia kunatokana na usimamizi, unajua kabisa nilikuwa niko mwenyewe kila kitu napiga mwenyewe, niko tu na ile family unajua family ambayo inaku support. Kwahiyo vitu vingi vinavyoendelea huwezi ukawa unavi-handle katika time, kwahiyo kuna muda unapita unataka kutoa kitu lakini je unatoaje hiki kitu, ndo maana mi inachukua muda mrefu lakini kama nikiweka nimeweka.” Alieleza Mavoko.

Pia Mavoko ameahidi kuachia video kali ya ya wimbo huo mpya hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents