Burudani

Rich Mavoko akanusha kufichwa ndani na mwanamke

Rich Mavoko amedai kuwa ukimya wake hautokani na kufichwa ndani na mwanamke kama baadhi ya watu wanavyoamini.

1977416_816482978391474_3724788443506466378_n

Akizungumza na E-Newz ya EATV jana, Mavoko alisema yeye binafsi hapendi hapendi kuweka sambamba muziki na maisha yake ya uhusiano.

“Kukaa kimya inategemea na kitu unachotaka kutoa. Muziki umekuwa biashara na ni biashara ya kujipanga,” alisema. “Kukaa kwangu kimya sina maana sina kazi ndani. Mimi ni mtu mzima siwezi nikasema kazi yangu niingize na mapenzi, itakuwa ni vitu viwili tofauti. Mambo yangu ya kawaida siwezi kuchanganya na muziki.”

“Halafu kusema mwanamke anaweza kunibana kwenye mambo yangu ya muziki huo ni uongo. Watu wanalalamika sana kwenye mitandao yangu ya kijamii kuhusu kazi, wanipe time, kwenye mwezi wa kumi mwishoni au mwezi wa 11 mwanzoni kazi mpya itatoka,” aliongeza staa huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents