Habari

Restless Development wazindua ilani mpya ya vijana 2015

Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya vijana nchini, Restless Development ikishirikiana na Tanzania Young Vision Association (TYVA), Youth of United Nations Association (YUNA), Femina, Salama Foundation, Tamasha, ZAFAYCO pamoja na Youth For Africa imezindua ilani mpya ya vijana 2015.

Nicas  Ngumba Programmer manager wa Restless Revelopment
Nicas Ngumba Program Manager wa Restless Revelopment

Akizungumza leo na vijana waliojitokeza kwenye uzinduzi huo uliofanyika ndani ya ukumbi wa Blue Pearl Hotel jijini Dar es Salaam, Meneja Mradi wa Restless Development, Nicas Ngumba alisema ilani hiyo imepatikana baada kuzunguka katika mikoa 11 ya Tanzania na kuzungumza na vijana waliotoa maoni juu ya matarajio ya serikali inayokuja.

“Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umoja wa asasi za vijana unaongozwa na Restless Development kwa kushirikiana na TYVA, FEMINA, SALAMA FOUNDATION, YOA, ZAFAYCO na YUNA umeungana na kukusanya maoni juu ya nini serikali tarajiwa inapaswa kufanya kwa upande wa vipaumbele vya vijana,” alisema. Mchakato huo ulihusisha uchunguzi wa taarifa mbalimbali na ukusanyaji wa maoni kutoka kwa vijana katika mikoa na wilaya mbalimbali kwa kutumia madodoso na vikundi vya majadiliano. Uchambuzi huu unaonyesha kuwa vipaumbele vya vijana ni pamoja na suala la ajira, elimu bora, huduma za vijana rafiki na vijana, ishiriki katika vyombo vya maamuzi, utawala bora na uwajibikaji, ushiriki na ulinzi wa rasilimali za nchi, ulinzi na ushiriki wa vijana na watu wenye ulemavu, usawa wa kijinsia, kulindwa kwa haki za michezo na sanaa pamoja na haki za vijana wa kitanzania katika mambo ya kimataifa,” alisema Ngumba.

Ngumba alisema maoni hayo yalikusanywa kutoka kwa vijana wenye elimu ya juu, vyuo pamoja na watu wasio na elimu.

Kwa upande waKE mwakilishi wa FEMINA, Amabilis Batamula alisema Femina Hip imekuwa mstari wa mbele kukaa na vijana na kuzungumza nao changamoto mbalimbali pamoja na kutoa elimu juu ya kujitambua.

Amabilis Batamula kutoka FEMINA Hip
Amabilis Batamula kutoka FEMINA Hip

“Fema imekuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi wa vijana, tumekuwa tukielimisha vijana mbalimbali kupita majarida yetu. Femina Hip pamoja na asasi za kiraia tunazoshirikiana nazo tunaamini kwamba mara nyingi wasichana wanatengwa katika ulingo wa siasa kutokana na tamaduni na desturi zetu, taratibu za kidini, dhana na mitazamo ya jamii, ubaguzi wa kijinsia, kiwango kidogo cha elimu, kutokuwa na taarifa, na athari za umasikini zinazowakumba wanawake, ili kujenga Tanzania njema, imara na itayokuwa,” alisema Amabilis Batamula.

Kwa upande wake naibu katibu mtendaji wa taasisi ya TYVA, Saddam Khalfan alisema katika uchukuaji wa maoni waligundua kuwa zaidi ya 80% ya vijana wamejiandikisha na wapo tayari kupiga kura.

“Unajua uchaguzi uliopita vijana wengi hawakupiga kura lakini mwaka huu wengi wameonyesha nia ya kutaka kupiga kura ili kuwapata viongozi wataowaletea maendeleo,” alisema.

Katika hatua nyingine baada ya uzinduzi huo wadau kama Mike Mushi ambaye ni mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums, Maria Sarungi Tsehaim mwanzilishi wa Change Tanzania, Adam Anthony wa program OSIEA, rapper Nick wa Pili, Lawrence Chuma, mwanzilishi wa Tanzania Bora Initiative pamoja na Dr Ally Possi ambaye ni mwanasheria walipata wasaa wa kuizungumzia ajenda ya (What do we want see in Tanzania in the coming five year?).

Maria Sarungi wanzilishi wa Change Tanzania
Maria Sarungi wanzilishi wa Change Tanzania

Dr Ally Possi akizungumza na vijana
Dr Ally Possi akizungumza na vijana

Lawrenc Chuma kutoka Tanzania Bora Initiative
Adam Anthony kutoka Open Society Initiative for Eastern Africa (OSIEA)

Margaret Mliwa
Margaret Mliwa wa Restless Development

Maria Sarungi akizungumza na wananchi

Mike Mushi akizungumza na vijana
Mike Mushi akizungumza na vijana

Msanii wa muziki Hip Hop Nikki wa Pili akizungumza na vijana

Vijana wa wakisikiliza kwa makini
Vijana wa wakisikiliza kwa makini

Vijana wakitoa waoni yao juu wa serikali ijayo
Vijana wakitoa waoni yao juu wa serikali ijayo

Vijana wakiwa wamejitokeza kwa wingi
Vijana wakiwa wamejitokeza kwa wingi


Wanafunzi kutoka Kambangwa
Wanafunzi kutoka Kambangwa sekondari

IMG_0279
IMG_0290

IMG_0294

IMG_0298

IMG_0305

IMG_0307

IMG_0309

IMG_0318

IMG_0329

IMG_0342

IMG_0344

IMG_0345

IMG_0352

IMG_0356

IMG_0359

IMG_0363

IMG_0364

IMG_0365

IMG_0366

IMG_0367

IMG_0369

IMG_0373

IMG_0375

IMG_0383

IMG_0393

IMG_0397

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents