Reina atabiri makubwa
Kipa wa Livrepool, Jose Manuel Reina, amaesema kubadili mmiliki wa klabu kutaifanya timu iwe bora.
Reina amekua na hasira kutokana na timu yake kutokuanza vizuri msimu huu ambapo kwasasa inashika nafasi ya tatu kutoka mkiani katika msimamo wa ligi.
Alisema hiki ni kipindi kigumu sana kwangu, tangu nilipojiunga klabu hii. Nadhani klabu ikiwa chini ya mmiliki mpya mambo yatakuwa mazuri zaidi.
Kampuni ya New England Sports Ventures (NESV), ambayo pia inamiliki timu ya mpira wa baseball ya Boston Red Sox wiki iliopita ilikubali kuinunua Liverpool kwa paund milioni 300 hata hivyo wamiliki Tom Hicks na George Gillett wanapinga uuuzaji wa klabu katika mahama kuu. Reina alisema ingawa mvutano huo unawachanganya wachezaji, sio sababu ya kufanya vibaya na timu kushika nafasi ya tatu kutoka mkiani.