Burudani

Redsan kuzindua albam na Keri Hilson

red_keri

Msanii  wa muziki kutoka nchini Kenya Swabri Mohamed aka Redsan, anarajia kuachia  Albamu yake April 13 Mwaka huu huku mwanadada kutoka nchini Marekani Kelly Hilson akitegemewa kushuka katika Jiji hilo la Nairobi kumpiga tafu.


Akizungumza na kurasa ya Bongo5, Redsan alisema mbali na Hilson, wasanii wengine watakaomsindikiza ni Ambwene Yessaya (AY), kutoka Tanzania.

Redsan alisema ana uhakika kuwa show hiyo itakuwa funika Bovu kwa kile alichodai kuwa maandalizi kabambe yaliyo tayari fanyika kwa ajili ya uzinduzi wa Albam hiyo.

Pia alisema mbali na uzinduzi huo hivi sasa anajiandaa kurekodi Track moja akimshirikisha mwanadada huyo Kelly, anayoisifia kuwa pia itakuwa moto wa kuotea mbali kwa kile alichodai kuwa ni track ya wakali watupu.

Amewataka Wabongo nao kujitokeza pale Jijini Nairobi siku hiyo kumpa shavu katika uzinduzi wake huo wa albam hiyo Mpya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents