Burudani

Recho azungumzia kolabo aliyofanya na Cassim Mganga

Recho Kizunguzungu amesema ameamua kukaa chini na msanii mwenzake anayesifika kwa kuimba nyimbo za mapenzi, Cassim Mganga kuandika wimbo mpya pamoja.

Recho (2)

Recho amesema maandalizi ya kazi hiyo yapo tayari na wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha kazi hiyo.

“Kuna nyimbo ambayo ipo kwa Lamar nimefanya na Cassim, inatarajiwa baada ya fiesta kumalizika nikaiachia,” Recho ameiambia Bongo5. “Recho ukimuangalia mapenzi na Cassim ndo usiseme. Kwahiyo hii nyimbo, sitaki hata kuongea. Nyimbo bado jina hatujaipa lakini nyimbo ipo na imeshakwisha kila kitu imebakia vitu vidogo ambavyo sio vya kwetu ni vya producer mwenyewe Lamar. Hii nyimbo pia itatoka na video tupo kwenye michakato ya maandalizi,” aliongeza.

Kwa upande mwingine Recho amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya video ya wimbo wake ‘Replay’ ambayo pia itatoka baada ya kumalizika kwa tour zake za show.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents