Burudani

Ray Kigosi: Tuache kuwadharau wasanii na kuwaona Kama hawastahili kuingia Kwenye Siasa

Vicent Kigosi a.k.a Ray amefunguka kuwa anasikitishwa na jinsi ambavyo baadhi ya watu wanawakatisha tamaa wasanii wa Tanzania wanapoamua kuingia kwenye siasa.

Ray

Muigizaji huyo wa filamu za Bongo ametoa yake ya moyoni kufuatia kile alichokiona baada ya muigizaji mwenzie, Irene Uwoya kushinda kura za maoni kwenye viti maalum UVCCM Tabora.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram hiki ndicho alichokiandika:

“Nimekaa Hapa Ofisini Kwangu Nikitafakari Mengi Sana kuhusu Baadhi Ya Watanzaia Kuwakatisha Tamaa Wasanii Wao Sasa Cjui Ni Roho Mbaya Ama Nini Maaana Leo Irene Uwoya Kashinda Kwenye Viti Maalum Tabora Lkn Coments Zimekuwa Nyingi Sana Kuwa Heti Baba Wa Taifa Nyanyuka Maana Chama Chako Kinaangamia. Hapana Hakuna Sehemu Yotote Inayopinga Mtu Kugombania Ubunge Maaana Ni Haki Ya Kila Mtanzania Mwenye Kukidhi VigezoYa Katiba Ya Nchi Ye2 .

Tuache Roho Mbaya Na Kuwadharau Wasanii Nakuwaona Kama Wa2 Wasiostahili Kuingia Kwenye Siasa Hivi Niulize Swali? Kuna Shule Yoyote Inayofundisha Siasa? Nadhani Kila m2 Atakuwa Na Jibu Lake Kichwani Tumeona Mifano Mingi 2 Kwa Wasanii Waliongia Kwenye Siasa Na wakafanikiwa Ndani Ya Africa Na Nje Ya Africa Marekani.

ARNOLD SCHWARZENEGGER GAVANA , DESMOND ELIOT MUIGIZAJI TOKA NIGERIA ALISHIDA PIA UGAVANA, PIA YUPO RICHARD MOFE DAMIJO WENGI WANAMJUA KWA JINA LA PASTOR OKEMY TOKA NIGERIA Pia Ni Gavana Nk. Why Sisi Tusithubutu Wapeni Nguvu Wasanii Wenu Na Kuwatia Moyo Pale Wanapothubutu Kufanya Jambo Lolote. Waswahili Wanasemaje Kulegalega C Kufa Kufa Ni Kuoza Utumbo. Utabaki Kuwa Mtazamo Wangu Over… “-Ray Kigosi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents