Bongo Movie

Ray, Irene Uwoya na Dulla (mjukuu wa Ambua) kuja na ‘Sister Marry’

Ray akiigiza kama padre

Wapenzi wa filamu za Vincent Kigosi aka Ray The Greatest wanatarajia kufurahi mwezi huu baada ya muongozaji na muigizaji huyo kuwa mbioni kuachia filamu mpya iitwayo ‘Sister Marry’.

Katika filamu hiyo Ray ameigiza kama padre huku Irene Uwoya akiigiza kama mtawa ambaye alilazimishwa kuingia kwenye shughuli hiyo bila hiari yake.

Watawa ambapo miongoni mwao yupo Irene Uwoya na Johari wakipata maelekezo kutoka kwa mkuu wao

Johari (Sista Beata)

Akiongea na Bongo5 leo kuhusiana na kisa kilichopo kwenye filamu hiyo, mtangazaji wa East Africa Television Abdallah Ambua aka Dulla, amesema yeye ameigiza kama Henry ambaye ni mpenzi wake na Irene Uwoya aliyeingia kwenye utawa.

Dulla akiwa kwenye scene kushuhudia mambo yanavyokwenda

Amesema filamu hiyo inajaribu kuonesha hali halisi ambapo masista wengi hujikuta wakivunja amri za utawa kwa kujihusisha na vitendo viovu ikiwa ni pamoja na kutembea na mapadre.

Ray akipitia script
Watawa

Dulla ameongeza kuwa Sister Marry inaweza kutoka mwezi huu ambapo Blandina ‘Johari’ Chagula naye ameigiza kama mtawa anayeitwa Sista Beata.

“Huu mzigo si mchezo subirini kwa hamu sana mara nyingi huwa sikosei kwenye kazi zangu ni sinema niliyotumia hela nyingi sana mpaka kuona hivi watu walivyo,” ameandika Ray kwenye blog yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents