Burudani

Ray C: Pole kaka yangu Chidi Benz, naumia kuona tatizo ulilokuwa nalo bado haujalitafutia jibu

Baada ya Chidi Benz kukamatwa na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini dar es salaam October 24 akielekea Mbeya (Ingia hapa), Rehema Chalamila wa taasisi ya Ray C Foundation amempa pole na kumwandikia ujumbe rapper huyo wa kutaka kumsaidia aachane na matumizi ya dawa hizo.

Rayc Chidi

Kupitia Instagram leo (October 25) Ray C amepost picha (hapo juu) na kuandika:

“Pole kaka yangu Chidi Benz, Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako, Mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo ulilonalo na Mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu!

Nadhani janga hili lililokukuta litakuwa Kama jibu kwako kwamba unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko ya madawa ya kulevya!!!!

Kama Mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe utaweza!!!!Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana !!Watanzania tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine na Unazuilika na Kutibika,Ana kipaji na Ana uwezo wa kurudi tena kwenye Sanaa,Tumuombee mema………Tanzania Stand Up n Wish Him Luck…………With Love,Ray C Foundation”

rayc

Ujumbe huo unakuja ikiwa ni miezi mitatu tangu Ray C kulalamika kuwa alipigwa na Chidi. July 10, 2014 Ray C aliiambia Bongo5 kuwa Chidi Benz alimvamia nyumbani kwake na kumpiga.

“Kweli alinivamia alhamisi usiku, amenipiga mimi na amenifanyia uharibifu wa mali. Mimi nilikuwa namtafuta kwasababu ya show ya kuelimisha vijana na maswala ya madawa ya kulevya, yeye akachukulia kivingine kabisa, nahisi amechanganyikiwa na madawa ya kulevya.” Alisema Ray C

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents