Burudani

Ray C Foundation yapanga kuanzisha kituo chake cha rehab kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya

Taasisi ya Ray C Foundation, inatarajia pamoja na mambo mengine, kuanzisha kituo chake cha rehab ili kuwasaidia vijana na watu wengine walioathirika na madawa ya kulevya nchini.

Ray C

Taasisi hiyo imeanzishwana mwanamuziki mkongwe nchini, Rehema Chalamila aka Ray C ambaye naye alikuwa muathirika wa madawa hayo ya kulevya lakini alifanikiwa kupata tiba iliyomsaidia kurejea kwenye afya yake ya kawaida. Rais Jakaya Kikwete alijitolea kugharamikia matibabu yake.

“Tunataka kuanzisha rehabilitation centre yetu wenyewe ambayo tutakuwa tunapokea waathirika, tunapata watu wa saikolojia wanakuja wanaongea nao kuwapa ushauri nasaha,” amesema Ray C.

Pia amesema taasisi yake itakuwa ikizunguka katika shule mbalimbali nchini kuongea na wanafunzi kuhusiana na madhara ya madawa ya kulevya pamoja na kufanya bonanza mbalimbali za uhamasishaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents