Burudani

Ray C Foundation yafungua mgahawa, itaajiri vijana waliojitoa kwenye matumizi ya dawa za kulevya

Taasisi ya Ray C Foundation iliyo chini ya muimbaji mkongwe, Ray C imefanikiwa kuongeza mradi mpya wa mgahawa ambao utatoa fursa ya ajira kwa vijana waliojikomboa kutoka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Mgawaha wa Ray C Foundation

Kupitia Instagram ya Ray C ameandika:

Matunda ya Ray C Foundation,Namshukuru Mungu kwa kuendelea kutubariki,kupitia foundation yetu tumeanza kufungua miradi mbalimbali ili kuwawezesha vijana walioamua kubadilika na kuachana na dawa za kulevya kupata ajira ili waweze kuendesha maisha!kwakuanza Ray C FOUNDATION imefungua mgahawa nje ya hospitali ya Mwananyamala ili kuwawezesha wagonjwa na wauguzi waweze kupata chakula cha kila aina na kitamu,mgahawa Wetu una chakula cha kila aina na tunachukua oda za harusi,kitchen party!msiba,birthday,mikutano nk.

Menu yetu pilau Kuku,wali Kuku,wali nyama,pilau Kuku,pilau Samaki,ugali Samaki,tambi na nyama ya kusaga,macaroni,beef burger,Shawarma,sambusa,Bagia za kunde,chapati,ugali wa muogo,kisamvu,bamia,mlenda,nyama chomaa,mbuzi choma,ndizi choma,urojo,ndizi bukoba/mshale,vitumbua,juice ya miwa,juice ya karoti,tikiti,juice ya avocado,.juice ya ukwaju,juice ya mango!!!chocolate cake,cake ya zabibu kavu,chapati za maji etc agiza chochote utaletewa hadi mlangoni pia tunafanya delivery nyumbani,maofisini na mikutanoni .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents