Burudani

Ray C atoa ufafanuzi juu ya uvumi wa kuzuiwa na serikali kwenda Mombasa kufanya show

Mwimbaji na mwana harakati wa kupambana na dawa za kulevya nchini, Rehema Chalamila a.k.a Ray C ametolea ufafanuzi taarifa zilizoripotiwa na mitandao ya Kenya, kuwa serikali ya Tanzania imemzuia kwenda Mombasa alikotarajiwa kufanya onesho la muziki.

Ray-C-710x434

Ray C ametoa sababu za kushindwa kwenda Mombasa kwa kusema “niko kwenye tiba ya methadone”, ameiambia EATV.

Ameongeza kuwa alishauriwa na madaktari kutoacha kutumia dozi, hivyo ikamlazimu asisafiri.

“…madaktari walinishauri kutokwenda nisiache dozi, niliongea na promota na nimwelewa sana. Tulijaribu pia kutaka kujua kama kule (Mombasa) kuna weza kupatikana methadone, nilijaribu kuulizia kama nikifika kule labda nikaumwa ghafla nikapata daktari, mpaka Jumamosi jioni nataka kukaribia kwenye ndege nikaambiwa hakuna tiba ya namna hiyo haijafika Mombasa kwahiyo nilishindwa kusafiri.” Alisema Ray C.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents