Burudani

Ray C asitisha kuachia wimbo mpya kufuatia msiba wa Aisha Madinda

Rehema Chalamila aka Ray C ameamua kuahirisha kuachia wimbo wake mpya kufuatia kifo cha mnenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda.

10831712_849605121756833_1879551915_n

Ray C ameiambia Bongo5 kuwa imembidi asitishe kusambaza wimbo huo ambao ulikuwa utoke leo na usambazwe kwenye vituo vyote vya radio.

“Nikiwa kama msanii kutokana na msiba wa msanii mwenzetu Aisha Madinda,” amesema. “Umesitisha utoaji wa single yangu mpya mpaka tutakapompumzishA. Kuna sehemu tayari nimekwishasambaza lakini nitaitoa ili tushirikiane kwa pamoja katika msiba huu na baada ya hapo utaweza kutoka,” ameongeza.

Aisha alipelekwa kwenye hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam Jumatano akiwa amefariki tayari.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents