Burudani

Ray C apania kurejesha kiuno chake kisicho na mfupa!

Miaka sita au saba iliyopita Rehema Chalamila aka Ray C alisifika kwa kukata mauno jukwaani kwa style ya belly dance au kama anavyocheza msanii mrembo wa Colombia, Shakira.

10832221_412060875637061_260882317_n

Na ndio maana alipewa jina ‘Kiuno Bila Mfupa’. Lakini hata hivyo baada ya kupona kutoka kwenye uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya na kuwa mwanaharakati namba moja wa vita dhidi yake, Ray C hana kiuno kisicho na mfupa tena. Ray C wa sasa ni mnene.

Good news kwa mashabiki wake ni kuwa si tu anajiandaa kuachia kazi yake mpya baada ya kukaa kimya kwa miaka mingi, bali pia anafanya kila awezalo ili arudishe umbo lake. Anachofanya Ray C kwa sasa ni kuhudhuria sana gym kukata weight kwa mazoezi makali lakini pia akitumia dawa ziitwazo Clean 9 zinazosaidia kupunguza uzito.

https://www.youtube.com/watch?v=tQ31O6YGdxM

Kupitia Instagram, Ray C alipost picha yake za enzi akiwa na umbo dogo na kuandika: his is me….huku clean 9 na kule gym so lazma body irudi.”

Kila lakheri Ray C kwenye safari yako ya kurejesha umbo lako la kuvutia.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents