Bongo Movie

Ray aliwahi kuwa dereva wa JB na Richie Richie

Safari ya kuwa muigizaji maarufu wa filamu haikuwa rahisi kwa Vincent Kigosi aka Ray. Muigizaji huyo amewahi kuwa dereva wa wasanii wenzie, JB na Richie lakini pia alikuwa mcheza ngoma kwenye kikundi cha Kaole.

Ray

“Cha msingi mimi ni msanii sio mbabaishaji katika suala zima la sanaa,” Ray alisema kwenye kipindi cha Kili Chat. “Niliingia pale Kaole Sanaa Group baada ya kutoka Nyota Academy. Kufika pale nikakuta watu wanacheza ngoma, nikasema kwa sababu mimi nilikuwa na passion unajua kazi hii kwanza uwe na passion usifanye kwa sababu upate umaarufu au upate pesa. Kazi kwanza uipende halafu umaarufu baadaye. Pesa muhimu sana lakini fanya kitu kwa passion,” aliongeza.

“Kwahiyo mimi nilivyoingia pale Kaole nikakuta kuna ngoma inachezwa lakini nikaona ngoma inachezwa sio professional kwahiyo nikatoa pesa yangu mfukoni nikamtafuta mwalimu akaanza kutufundisha ngoma. Kwa sababu mimi nilikuwa napenda ngoma nikaanza kucheza ngoma lakini wasanii wengine pale wakubwa wakawa wanashangaa, nafika saa nne asubuhi napasha ngoma zangu moto, kikundi kikawa kikubwa sana nikapata mwaliko wa kwenda Dubai, nikakwea pipa wasanii wakaanza majungu ‘haaa! kwanii aende yeye, lakini mwanzo walikuwa wanasema ‘huyu jamaa anajihangaisha.”

Katika hatua nyingine Ray alisema kuwa haikuwa rahisi kuingia kwenye filamu kwani alianza kuwa dereva JB na Richie.

“Mimi sanaa hii nipo au nilianza kama mwaka wa 15 iliyopita, si kumi na tano ndo nimeanza kufahamika. Nilianza kwenye vikundi vya chini. Kikundi changu cha kwanza kilikuwa kinaitwa Super Noval Culture Group, kama cha kwangu, lakini watu walikimbia kwa sababu unajua target za wasanii wengi wanaokuja wachanga wanataka kuonekana kwenye TV, wawe maarufu. Lakini mimi niliendelea kuvumilia nikaenda sehemu Nyota Academy nikawa dereva wa JB na Single Mtambalike ‘Richie Richie’ niwapeleke tu mazoeni kwao nishuke niwaangalie wanavyoenda kufanya mazoezi. Lakini baadaye Single Mtambalike akaniambia ‘Ray kwanini wewe usiigize, mwonekano wako mzuri kwanini usiigize! Ndo nikaamua kuingia Nyota Academy ndo safari yangu ya maisha ilipoanzia pale.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents