Michezo

Rashford ndani ya kikosi cha Uingereza UERO 2016

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amesema anaweza akamuingiza Rashford kwenye kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya Euro itakayofanyika Paris mwaka huu.

03_04000840_86384c_2722727a

Hodgson amesema, “Ninaweza nikamuita au nisimuite, naamini atafanya vizuri. Kwa baadae, niliwapa nafasi vijana kwa kuingiza kikosini na wakafanya vizuri kama. Oxlade-Chamberlain nilimuita 2012, Sterling nilimchukua akiwa na umri wa miaka 18 au 19 na Ross Barkley nayeye pia.”

“Nimekuwa nikimuangalia Rashford tangu miaka miwili iliyopita, amechezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18,” aliongezea Hodgson.

Lakini pia Rashford ataichezea timu ya Uingereza U-21 mwishoni mwa mwezi huu timu hiyo itakapochezana na Switzerland.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents