Bongo5 MakalaBurudani

Rappers 20 wa Tanzania walioitawala robo tatu ya mwaka 2014 (TV, Redio na Shows)

Wasanii wa hiphop wanaunda sehemu kubwa na ya muhimu katika muziki wa Tanzania. Japo kuna watu wanaoamini kuwa ushindani kati ya rappers wa Tanzania umepungua ukilinganisha na wasanii wa kuimba, bado tumeshuhudia ngoma nyingi na kali zimetoka hadi wiki ya kwanza ya mwezi October 2014. Hawa ni wasanii 20 wa hip hop Tanzania waliosikika zaidi kwenye redio, kuonekana zaidi kwenye TV, kufanya show nyingi ama nyimbo zao kusikilizwa, kutazamwa na kuongelewa zaidi mtandaoni katika robo tatu ya mwaka huu.

1. Joh Makini

Hakuna ubishi kuwa mwaka 2014 ulitawaliwa na Weusi. Kundi/kampuni hii kutoka Arusha imekuwa ikifanya kazi na kuachia jiwe baada ya jiwe bila kupumzika. Hata hivyo kazi kubwa zaidi imefanywa na mwamba wa kaskazini ambaye mwaka huu amekuwa rapper pekee kutoka Tanzania kushiriki kwenye kipindi cha Coke Studio Africa. Pamoja na kufanya vizuri na anthem za Weusi, ‘Gere’ iliyoshuhudia wasanii hao wakisafiri hadi Kenya kwenda kushoot video yake pamoja na video ya ‘Nje ya Box’ iliyokuwa video yao ya kwanza kuwahi kuchezwa Channel O, Joh amefanya vizuri mwaka huu na wimbo wake ‘I See Me’ ambao video yake iliyoongozwa na Mkenya Enos Olik, itatoka hivi karibuni.

Joh ameendelea kuwa msanii wa hip hop anayetafutwa zaidi kwa collabo kwa sasa akiwa ameshirikishwa kwenye msululu wa hits za mwaka huu ikiwemo ‘Unanichora’ ya Ben Pol, ‘Ni Penzi’ ya Damian Soul, ngoma ya Belle 9 iliyotoka hivi karibuni ‘Vitamin Music’ na zingine. Upande wa show, ukimtoa Nay wa Mitego, hakuna msanii wa hip hop aliyepiga show nyingi kama huyu jamaa.

2. Mwana FA

IMG_9873

Ilimchukua Mwana FA muda kiasi baada ya kutoa ‘Kama Zamani’, kuachia ngoma nyingine ya peke yake. Akiwa na ngoma nyingi kibindoni, alizorekodi kitambo na mpya, FA alijikuta njia panda kuchagua kutoa kati ya wimbo aliomshirikisha Alikiba na kutayarishwa na Marco Chali au ‘Mfalme’ aliyomshirikisha G-Nako na kupikwa na Nahreel. Bahati iliiangukia ‘Mfalme’ ambayo ilikuja kumuongezea orodha ya hits zilizoshika nafasi ya kwanza kwenye vituo vingi vya redio. Baada ya video ya wimbo wake na AY ‘Bila Kukunja Goti’, FA hajaonekana tena kwenye video mpya. Ni video ya ‘Mfalme’ aliyofanya na Mkenya Kevin Bosco Junior ndio itakuja kukata kiu ya mashabiki wake wanaomngoja kumuona tena kwenye video mpya.

3. Young Killer

Mr Blue anakiri kuwa uwezo wa Young Killer kiuandishi ni hatari kuliko umri wake. Ni kweli, rapper huyo wa Mwanza ameendelea kupata salute si tu kutoka kwa mashabiki wake, bali pia kwa rappers wakongwe wanaoheshimika.

https://www.youtube.com/watch?v=8Xd6OhvHyNs

Mwaka 2014, dogo huyu ameendelea kuuza ujuzi wake redioni kwa ngoma zake ‘My Power’ iliyo na video yake tayari na ‘Umebadilika’ ambayo alimshirikisha Banana Zorro. Video ya wimbo huo imeshafanyika na ipo kwenye maandalizi ya mwisho, chini ya muongozaji Hefemi. Katika kuashiria kuwa miezi miwili ya mwaka 2014 itabakia kuwa mizuri kwake, rapper huyo ameingia location kushoot video ya hit ijayo ‘13’ aliyomshirikisha kaka yake kimuziki, Fareed Kubanda aka Fid Q na muongozaji akiwa Nisher.

10724955_558184617661703_514903870_n

4. Professor Jay

Professor Jay aka ‘Underground Mzee’ anasema kwa sasa ana hasira kama msanii mpya anayehangaika kutoka. “Ukiwa na hasira kama underground maana yake unataka kutoka. Professor anataka kutoka kwenye level nyingine ya international kwasababu mimi najua me I am the best. Lakini kwasababu nimelemaa, nimekaa muda mwingi sasa ni muda wa kufanya mabadiliko,” aliiambia Bongo5 hivi karibuni.

Katika kuashiria kuwa hataki tena mchezo, hivi karibuni rapper huyo mkongwe aliachia video mbili kwa mpigo. ‘Kipi Sijasikia’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz na kuongozwa na Adam Juma na ‘3 Chafu’ iliyoongozwa na Hefemi. Kuna mengi ya kutarajia kutoka kwa rapper huyu ambaye anamiliki studio yake, Mwanalizombe Records.

5. Nay wa Mitego

Emmanuel Elibariki ametoka kuwa rapper aliyechukuliwa kama ‘mporokaji’ hadi kuwa mwana hiphop mwenye mafanikio makubwa. Akiwa na mjengo wake wa gharama kubwa na magari kadhaa, Nay ametisha sana katika kipindi cha miezi 10 iliyopita. Hits zake ‘Nakula Ujana’ na ‘Mr Nay’ ambazo zote zilifanyika Kenya, zimeendelea kumweka sehemu nzuri. Sijasahau pia collabo yake na Stamina ‘Kwenu Vipi’ ambayo kwenye show za Fiesta imekuwa ikishangiliwa ile mbaya.

6. Nick wa Pili

Kupitia moto wa kundi la Weusi, Nick amefanikiwa kuendelea kuwa ‘relevant’ huku pia akijichukulia heshima kubwa kwa harakati zake kama msomi wa shahada mbili. Pamoja na miradi ya Weusi, Nick wa Pili alifanikiwa kupata ‘mention’ bungeni kutokana na wimbo wake ‘Sitaki Kazi’ aliomshirikisha Ben Pol. Akiwa na Weusi wenzake, Nick amepanda kutumbuiza kwenye show nyingi kubwa za mwaka huu ikiwemo ziara ya Kilimanjaro na Fiesta.

7. Izzo B

Ukiwatoa Weusi, rapper huyu kutoka Mbeya ameendelea kuelekeza nguvu zake nyingi katika kuzifanyia video nyimbo zake. Mwaka huu Izzo amefanikiwa kutengeneza anthem mbili, Tummoghele na Walalahoi ambazo zote zimepikwa na producer anayekuja kwa kasi, Duppy.

8. AY

https://www.youtube.com/watch?v=MMbKKWvtnyM

Pamoja na kuwa na mafanikio mengi kibiashara, Ambwene Yesaya hajaonesha dalili za kupunguza speed. Mwaka huu amefanikiwa kutoa hit ‘Asante’ ambayo haijashia kushika chart nyingi za redio na TV za Tanzania pekee, bali pia vituo vya redio vya Kenya, Uganda, Rwanda na Nigeria. Rapper huyu mkongwe anasafiri hadi Marekani kwenda kushoot video ya ngoma yake ‘It’s Going Down’ aliyowashirikisha Lamyia Good na Ms Trinity.

9. Fid Q

Fid Q alimake headlines sana mwaka huu baada ya kushinda tuzo mbili za KTMA baada ya kukaa miaka kibao bila kupata. Nyimbo zilizomfanya asikike mwaka huu ni ‘Jipe Shavu’ aliyofanya na AY (mwishoni mwaka mwaka 2013) ambayo bahati mbaya video yake waliyokuwa wameshoot tayari haikutoka baada ya muongozaji Kevin Bosco Junior kuibiwa material. ‘Bongo Hiphop’ aliyomshirikisha P-Funk Majani ndio wimbo wake mpya. Hata hivyo kabla ya hapo alikuwa amewahi kuahidi kutoa wimbo uliotayarishwa na Majani lakini haikuwa hivyo.

Mwana FA, Fid Q, AY, Arthur na mshikaji

“Siku tatu kabla sijarelease (P-Funk) akaacha kuwa anapokea simu yangu. Lakini uzuri mimi tayari nilishajipack nina madude mengi tu ndani kwangu huwa yamekaa, basi nikaanza kupitia tu stock. Sikupitia hata nyingi, nilipitia kama tatu nikakutana na ‘Siri ya Mchezo’ nikaiona hii inaweza ikawafaa nikaitoa,” Fid alikiambia kituo cha Citizen Radio cha Kenya mwishoni mwa mwaka jana.
“Hakuwa amependa alichokuwa amemix,” Fid alisema kuelezea sababu ya Majani kutopokea simu yake.

“Unajua P-Funk ni ‘perfectionist’. Sio kwamba alikuwa ananidisrepect au nini. Hatoi kitu mpaka awe nacho comfortable, huwa anapenda kujiridhisha yeye mwenyewe kwanza. Nilijisikia vibaya lakini nikaja kugundua kuwa, nikijisikia vibaya sana naweza nikajikuta namchukia jamaa wakati kiukweli jamaa he picked me out of the ground, amenifanyia album ya kwanza kipindi ambacho hakukuwa na producer ambaye alikuwa tayari kunifanyia albam ya kwanza sababu walikuwa wanasema kwamba ‘I was too hardcore for mainstream’.

10. D-Knob

https://www.youtube.com/watch?v=z7HLpUUDJbA

Innocent Sahani aka D-Knob aliuvunja ukimya wake wa miaka mingi mwaka huu kwa kuachia anthem yake, ‘Nishike Mkono’ iliyotayarishwa na producer wa Mwanalizombe Studios, Villy. Nishike Mkono aliyomshirikisha Mwasiti ilimrudisha vyema rapper huyu wa Mtaani.com na kurejesha tena heshima yake kama miongoni mwa rappers wakali wa Tanzania. Aliachia pia ngoma nyingi, Njaa ya Mkwanja ambayo pia imekuwa na mafanikio.

11. Mr Blue

Japo wimbo wake ‘Pesa’ ulitoka tangu September mwaka jana, uliendelea kufanya vizuri mwaka huu na pia video yake ikiendelea kusubiriwa kwa hamu. Kwa mujibu wa mtangazaji wa Clouds FM, B12, Pesa ndio wimbo uliokuwa ukishangiliwa zaidi kwenye show za Fiesta. Pia watu wengi wanaamini kuwa Blue ndiye msanii aliyefanya vizuri zaidi kwenye show hizo. Pia ameendelea kusikika na kuonekana zaidi kwenye miradi ya click yake ya Micharazo.

12. G-Nako

Gnako Insta

Mwana FA anaamini kuwa G-Nako ndiye msanii mkali zaidi kwenye chorus na ndio maana aliamua kumshirikisha kwenye ‘Mfalme’, uamuzi uliokuwa sahihi. Na FA aliwahi kukiri kuwa ni G-Nako ndiye aliyekuwa na mchango mkubwa wa kuipendezesha hit hiyo.

“Actually kazi aliyoifanya G-Nako ndio imenyoosha kila kitu. Idea yangu niliyokuwa nayo ilikuwa tofauti kabisa. Nimeenda studio, G-Nako alivyofanya chorus i had to take beat na chorus sasa niende nikaandike upya. Verse ya kwanza nilikuwa na verse nyingine nilirekodi nikaiondoa, nikaweka verse nyingine nikaiondoa, hii ambayo unaisikia ipo humo ni ya tatu,” alisema.

Kupitia miradi ya Weusi, G-Nako amekuwa akitumiwa kama muimbaji mzuri wa chorus zao na kwa alichokifanya kwenye Nje ya Box na Gere, ni vigumu kukibeza kipaji chake. Kwa sasa rapper huyo ana nyimbo mbili mpya zinazoendelea kutafuta nafasi ya kujitengeneza kuwa hits ukiwemo Mavijanaa aliomshirikisha Nick wa Pili.

13. Shettah

https://www.youtube.com/watch?v=AC_mdKcJuNE

Baba huyu wa mtoto wa kike aitwaye Qayllah, aliamua kujipiga na kwenda kushoot video ya wimbo aliomshirikisha Diamond Platnumz, ‘Kerewa’ nchini Afrika Kusini. Uamuzi huo ulikuwa sahihi kwakuwa ngoma yake hiyo ilifanikiwa kuingia kwenye chart ya redio tatu za Nigeria. Wimbo huo uliingia kwenye Top 10 ya Naija 102.7 FM, City 105.1 FM na The Beat 99.9 FM zote za Nigeria. Video yake iliyoongozwa na Godfather nayo imefanikiwa kuchezwa kwenye TV kubwa ukiwemo MTV Base. Pia amefanikiwa kupata connections zaidi.

14. Stamina

https://www.youtube.com/watch?v=SrbQDQwdEvE

Mwaka huu Stamina amesikika kwenye ngoma yake ‘Mguu Pande, Mguu Sawa’ aliomshirikisha Walter Chilambo na pia wimbo alioshirikishwa na Joh Maker ‘Wanasemaje’ unaopata airplay nzuri kwenye TV. Sijasahau kuwa wimbo aliofanya na Nay wa Mitego ‘Kwenu Vipi’ ndio uliomrudisha vizuri mkali huyu wa steji aliyepewa nyota 5 za Fid Q.

“Mimi sasa hivi nimekuwa shabiki wa Stamina, tangu Fiesta imeanza mpaka lipofikia hapa wasanii wengi wanafanya vizuri lakini Stamina anafanya vizuri zaidi. Kwenye ukweli huwa nasema ukweli hiyo ndio Hip Hop, reality au uhalisia. Unajua tunasemaga tunawalisha uhalisia ili waucheuwe uhalisia wa mambo, ndo Hip Hop ilivyo. Huyu ni msanii tangu Fiesta inaanza mpaka inaisha hakuna hoo! sijui nilikuwa nimelala nimechelewa kupandishwa, sijui nimepandishwa mwisho huyu guarantee nasepa na kijiji,” alisema Fid.

15. Godzilla

Godzilla akisikiliza mashabiki wanavyo imba

You and I aliomshirikisha Marco Chali ndio wimbo wa Godzilla uliopata airtime kubwa zaidi mwaka huu. Pamoja na ngoma hiyo, Godzilla amesikika kwenye nyimbo kutoka katika mixtape yake Zillax iliyotoka January 5 mwaka huu. Tungi ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri kutoka kwenye mixtape hiyo. Hivi karibuni pia, Zizi na Diamond walisikika kwenye wimbo wa Zachaa, Mtoto wa Mama.

16. Young Dee

https://www.youtube.com/watch?v=99iV2Z8fdn4

Young Dee amefanya vizuri mwaka huu na ngoma kadhaa zikiwemo ‘Fununu’ aliomshirikisha Mwana FA, Rock Star ambayo video yake iliongozwa na Enos Olik pamoja na ‘Sio Mchoyo’ aliomshirikisha Jux.

17. Wakazi

Wakazi ambaye aliachia ngoma mbili, Sexy Lady f/ Jokate na ‘Sumu ya Panya’ ambayo video yake iliongozwa na Hefemi, anaamini anachukuliwa poa.

“Sijasema nataka kuitwa legend, sijataka kuitwa mkongwe, sijataka kuitwa king, sijataka kuitwa vyovyote, ila nilikuwa nataka tu nipate respect ile ambayo nastahili kutokana na what I have been fighting for as far as huu muziki wetu wa hip hop,” Wakazi aliiambia Bongo5. “And I don’t believe from just the explanation kwamba wasanii wenzangu wananichukulia poa hiyo tu ni tayari they are fighting against me kama vile am not part of this hiphop thing ambayo wote tunajaribu kufight for.” Wakazi ambaye kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha studio yake, anatarajia kuachia video ya wimbo wake ‘Wanawake wa Dar’ iliyoongozwa na Hefemi.

18. Kala Jeremiah

Ni wazi kuwa baada ya ‘Dear God’ iliyompa tuzo za KTMA, Kala anaendelea kujaribu kurejea kwenye kilele alichowekwa na hit hiyo. Mwaka huu amesikika kwenye remix ya Wale Wale aliowashirikisha Young Killer na Juma Nature iliyotoka na video yake pamoja na ‘Simu ya Mwisho’ aliyowashirikisha Mo Music na Nay wa Mitego.

19. Gosby

Gosby ndiye msanii wa kwanza wa Tanzania (ukimtoa Rose Muhando) kuwa na akaunti ya Vevo aliyoufungua kwa video yake ya ‘Baby Making Swag’ iliyotoka January mwaka huu. Wimbo wake wa kwanza kutoka tangu ajiondoe B’Hits ni ‘Maumivu’ aliomshirikisha Ommy Dimpoz. Akiwa anatarajia kuachia mixtape yake, MissTape, mwezi huu Gosby ameachia single iitwayo ‘Blame On Me’ aliomshirikisha Godzilla.

20.Nikki Mbishi

https://www.youtube.com/watch?v=yJml_1p0WKs

Nikki Mbishi ameendelea kufanya underground hip hop bila kuchoka na mwaka huu amefanikiwa kutoa nyimbo kadhaa zilizopata airtime kiasi japo zimefanya vizuri mtandaoni. Nyimbo hizo ni pamoja na Pesa Kwanza iliyokuja na video yake, Utamwambia Nini, Natoka Tanzania, Michepuko, Hands Down Low, Serikali ni Nini? Na Feel Alright. Hivi karibuni ataachia wimbo aliowashirikisha Lady Jaydee, One na Songa ‘Kupanda na Kushuka’.

Bonus:

Roma

Licha ya kutoa wimbo wake ‘KKK’ na ‘Maumivu’ aliofanya na Bob Junior, mwaka huu Roma hajatikisa kama miaka miwili iliyopita. Pamoja na hivyo, bado ameendelea kuitwa kwenye show nyingi na amekuwa akipagawisha kama kawaida.

Country Boy

https://www.youtube.com/watch?v=BWf8_1MwEok

Country Boy ni miongoni mwa wasanii wanaochukuliwa poa licha ya kuwa na uwezo wa aina yake. Mwaka huu ameonekana kwenye video ya My Clique aliofanya na Julio ‘Akili za Usiku’ aliowashirikisha Young Killer na Young Dee na pia single kama ‘Mchaka Mchaka’ aliomshirikisha Mr Blue na wimbo mpya aliofanya na kaka yake Babuu wa Kitaa, Kigangster Kisharobaro.

Songa

Rapper huyu wa Tamaduni Muzik ameendeela kujichukulia heshima kutokana na uandishi wake mahiri licha ya ukweli kuwa nyimbo zake huziskii sana redioni. Mwaka huu alitoa ngoma kadhaa zenye simulizi ikiwemo ‘Usiku’, ‘Ndege’ na ‘Enzi za Utoto’. Pia aliachia video ya wimbo wake ‘Kikosi cha Mizinga’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents