Habari

Rapper Wakazi Wasira awakingia kifua dada zake waliojiunga na CHADEMA

Wakazi

Baada ya watoto wa kaka yake na Waziri wa nchi ofisi ya rais mahusiano na uratibu Mheshimiwa Stephen Wasira kuchukua kadi za uanachama wa CHADEMA, kaka yao ambaye ni rapper aishiye nchini Marekani Wakazi Wasira amewakingia kifua dada yake.

Hiyo ni baada ya Esther na Lilian Wasira kuanza kushambuliwa kuwa wamemsaliti baba yao.

“Mimi ninawaunga Mkono wadogo zangu Lilian na Esther Wasira kwa kuamua kuchukua Kadi za Uanachama wa CHADEMA. Tanzania ni Nchi huru na kila mtu ana uhuru wa ku make decisions ambazo anaona zina manufaa kwake. ILA inabidi niwakumbushe nyie W****VU mnaoongea UPUUZI, CHADEMA kimeanzishwa na (including others) BOB MAKANI, EDWIN MTEI, MZEE NGWILULUPI na GEORGE B. WASSIRA, ambaye ni Baba Mzazi wa ESTHER, LILY na Wakazi. So what they did is basically follow “Dreams of their Father” na sio Kumuweka Baba Yao Mdogo STEVEN WASIRA kwenye kitimoto au Kumuaibisha. so all ya’ll mnaosema sijui usnitch sijui vitu vitu gani, STFU and get yaselves some bidness!!!! One,” aliandika Wakazi.

Esther na Lilian Wasira wakipokea kadi za uanachama kutoka kwa katibu mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa

Katika hatua nyingine jana mheshimiwa Wasira amesema watoto hao waliojiunga na CHADEMA kuwa si watoto wake wa kuzaa bali ni watoto wa ndugu yake ambao wana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa hapa nchini.

Kauli hiyo hata hivyo imetafsiriwa vibaya na watu wengi wanaodai kuwa amewakana.

“Mimi binafsi naona kajikanyaga tu kwa ili Mhe. WASIRA kwa sababu yeye kama baba mdogo pia mwana ukoo basi ni dhahiri na wazi ya kuwa ni watoto wake wala ilo halina ubishi kwa kuwa yeye kama baba-mdogo bado ana mamlaka juu ya watoto wale kwa namna moja au nyingine hivyo hakuna alilojitetea hapa,” aliandika mchangiaji mmoja kwenye ukurasa wa Facebook wa kituo cha ITV.

“Kwani watoto wake wa kuzaa wenyewe hawana haki!? kwani wao wamemwambia wamejiunga kwakuwa yeye ni baba yao mdogo?au aibu ndo imekufanya useme? yaani hata kwenu hukubaliki?inawezekana hata mkeo hasemi tu,atakuwa chadema na yeye sema kwako yupo kwa ajili ya ankara tu!” aliandika mwingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents