Burudani

Rapper Stopa Rhymes aanzisha kipindi chake cha Tv cha mapishi ‘Jirambe’

Rapper wa Arusha, Stopa Rhymes a.k.a Yokoi ameanzisha kipindi kipya cha TV kinachohusu mapishi. Kipindi hicho kinachoruka kupitia Azam TV kinaitwa ‘Jirambe’.

stopa2

Nimepiga story na Stopa ambaye ameelezea jinsi wazo la kuanzisha kipindi hicho lilivyokuja.

“Mwaka jana mwezi wa nane Tarehe 27/28/29 tulikua tunashoot Video ya Joslin ‘Tesa Nae’ sasa kuna namna jamaa Dir aliona kuna kitu tunaweza fanya so akanipa wazi tukali develope kufikia hatua ya kuanza production then tukapeleka Tv ikakubalika ndio tunafanya hadi sasa”.- Stopa

Stopa amesema kuwa baada ya kupata wazo hilo kutoka kwa wenzake, ilikuwa rahisi yeye kulipitisha na kuanza kulifanyia kazi kutokana na kuwa yeye mwenyewe anapenda kupika.

“Napenda kupika na huwa napika ndio maana Hata Idea ya mapishi nikaipenda na kuongezea ubunifu ili lisiwe Normal…sina ujuzi wa kupika profecionally ila passion tu.”

stopa na barnaba
Stopa akiwa na Barnaba kwenye ‘Jirambe’

Akielezea kuhusu kipindi cha Jirambe:

“Kinahusisha watu mashuhuri/maarufu kwenye nyanja mbali mbali kikubwa mtu awe anajulikana ili pindi akiwa kwenye program watu wapate hamu ya kujua mambo toka kwake hususan mapishi.

Tunaanzia jikoni then tunakua tunefungua kipindi ndipo Mgeni anasema anachotaka kupika alafu tunaenda Sokoni tukirudi ni kupika na kula na kupiga stori alafu tunaaga.”

Ameongeza kuwa licha ya kuwa yeye ndiye anayeongoza kipindi hicho lakini kuna watu wengine wawili anaoshirikiana nao ambao ni director na mtu wa settings.

Mashabiki wa Stopa bado wataendelea kupata kazi zake za muziki kwasababu hajaacha kufanya muziki, na anatarajia kuachia single tatu mpya hivi karibuni.

“Muziki bado nafanya kama kawaida…napanga muda wa Tv Show na muda ajili ya Music,so production huwa weekdays zaidi hivyo vile mambo ya shows mostly ni Wekend nakua free,na hata Music Recording nafanya zaidi usiku… Soon nita release ngoma tatu kwa pamoja…”

Tazama baadhi ya vipindi vya Stopa akiwa na mastaa katika Jirambe;

https://youtu.be/slvdPhsWKiU

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents