Burudani

Rapper Slim Sal (Bongo) azungumza alivyojisikia baada ya kundi la UK ‘Little Mix’ kutumia idea yake

Inaweza kuwa ni mgongano wa idea ama kundi la muziki lenye mafanikio makubwa nchini Uingereza, Little Mix limeiga idea ya wimbo wa rapper wa Bongo, Slim Sal?

Wimbo wa Slim Sal uitwao Tumpigie Makofi una idea ile ile kama ya wimbo wa Little Mix Shout to My EX. Kwenye wimbo wa Slim, anaimba kwenye chorus, “Thanks to to my ex girlfriend shout to my ex girl.”

https://www.youtube.com/watch?v=LIwjRoZyLTo&feature=youtu.be

Cha kushangaza ni kuwa wimbo wa Slim ulitoka February 12, 2016 na ule wa Little Mix ulitoka October 20, 2016.

“Sikujudge moja kwa moja lakini nafahamu dunia kijiji,” Slim ameiambia Bongo5 kuhusiana na alivyojisikia baada ya kuusikia wimbo wa Little Mix.

“Muandishi wa nyimbo inawezekana alisikia akavutiwa. Inanifanya nizidi kuamini kuwa watu wakiniambia muziki wangu si wa hapa au wengine husema im so ahead of time. Pia inanifanya nijione nipo vizuri kisanaa, kimawazo na hata as Creative Copywriter (my office position) nizidi kujikubali kuwa nina mawazo ya ki creative haswa,” ameongeza rapper huyo.

Hata hivyo siku za hivi karibuni, Slim ameamua kuwa mkimya kiasi cha watu kuhisi ameachana na muziki.

“Fans hawaelewi mazingira ya muziki kwa wasanii wa aina kama mimi, Gosby nk yapoje,” anasema.

https://www.youtube.com/watch?v=27SlkTZ_5yM

“Ningeweza kukomaa kama wanavyokomaa wenzangu yaani kutoa materials kila kukicha lakini nahisi nitapoteza Legacy yangu na watu wataaminishwa kuwa mimi ni msanii wa kutoa ngoma tu. Yaani inakuwa ni kawaida tu bila kupima thamani ya kazi zangu.”

https://www.youtube.com/watch?v=B3nj8ptRSkc

“They dont know mwaka 2015 nilikuwa na wimbo bora POSITIVE kuliko msanii yoyote Tanzania pengine East Africa (SHAURI YAKO ft G Nako). They dont know im the fastest rapper ever in Tanzania (No Silence)., Mistaripedia. They dont see the highest level of creativity kwenye rap.”

https://www.youtube.com/watch?v=55jbYKodW2I&feature=youtu.be

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents