Burudani

Rapper King Kaka ataja sababu ya kuachia ‘Senzenina’

By  | 

King Kaka amefunguka sababu ya kuachia wimbo wake mpya ‘Senzenina’ aliowashirikisha RedFourth Chorus.

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa amepoteza watu muhimu kwenye maisha yake na Senzenina ni neno lenye asili ya Afrika Kusini kutoka kabila la Xhosa/Zulu ambapo wimbo wake unaimbwa wakati wa msiba. “Kaka yangu alimpoteza mwanae mwaka jana, iliniathiri sana hilo. Nimepoteza marafiki wengi na familia ambao walikuwa muhimu kwangu. Kwanini wameondoka? Wimbo huu ni njia niliyotumia kuongea nao, uko wapi?,” amesema King Kaka.

Video ya wimbo huo imeongozwa na J. Blessing kutoka kampuni ya Link Global. Tazama hapa chini.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments