Burudani

Rapper King Kaka aachia video ya wimbo mpya, ataja maana ya wimbo huo

Baada ya kuanza mwaka 2017 kwa kuachia ‘Senzenina’, King Kaka kutoka Kenya ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Milele’ ambao amemshirikisha Pascal Tokodi na amefunguka maana ya jina hilo kwenye wimbo huo.

Rapper huyo ameiambia Bongo5, “Naamini hakuna mdundo wa upendo, ila huleta watu pamoja. Amri iliyo kuu katika biblia ni upendo. hadithi zote za upendo lazima zitabaki milele. Na hivyo ndio jinsi milele ulitokea.”

Naye Pascal Tokodi ambaye ameshirikishwa katika wimbo huo amesema, “Kwangu kufanya kazi na King Kaka imekuwa ni zaidi ya kolabo. Amefanikiwa zaidi katika muziki ni heshima kufanya kazi na kujifunza kutoka kwake. Naangalia mbele uwezekano wa kufanya naye kazi tena.”

Tazama video ya wimbo huo hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents