Bongo5 Makala

Random Thoughts: Hatuwezi kufanya biashara zingine zaidi ya kuuza t-shirt zenye maandishi ya single tunazotoa?

Unakumbuka kile kipindi kila msanii alikuwa akimiliki duka la nguo? Well, sio kila msanii alikuwa na duka lake lakini ni kweli wengi walianzisha maduka yao. Kwa sasa ni wachache waliobaki katika biashara hiyo kwakuwa wengi maduka yao yaliishia kuwapa stress tu zaidi ya neema waliyokuwa wakitegemea kuipata. Dawa ya biashara isiyokuwa na faida ni kuifunga tu, na wengi walifanya hivyo.

black_mens_t_shirt_funny_sayings-r6f38a022c8634e1097dc9050fb3f744e_va6px_512

Hata hivyo kwa sasa imeibuka biashara nyingine maarufu inayowafanywa na wasanii wengi, nayo ni kuuza t-shirt zenye majina ya single mpya. Sikatai ni kitu kizuri kwakuwa ni njia moja wapo ya kupromote single mpya. Lakini kibiashara kwangu naichukulia kama ‘idea cheap’ sana ya kijasiriamali tena kufanywa na msanii mkubwa wenye mashabiki wengi.

Nahisi kwa lengo la kupromote single, ningeelewa kama zingekuwa zinatengenezwa t-shirt kadhaa na ambazo msanii angezigawa bure kwa mashabiki wake wa damu. Unajua tatizo ni kwamba t-shirt zenye majina ya single hazidumu kwakuwa pale single inapopotea au inapochuja, inakuwa haina maana tena na kuivaa t-shirt yenye jina lililopitwa na wakati ni ushamba fulani hivi au sio?

Kama t-shirt hizo zinatengenezwa kwaajili ya promotion na sio kibiashara, hilo sio tatizo kwakuwa ukitoa single nyingine, ya zamani unaweza kuitupa na kuanza kushughulika na mpya.

Sitaki kuamini kama biashara ya t-shirt zenye majina ya single inalipa kivile ukizingatia kuwa ni t-shirt za msimu tu. Nadhani kama wasanii wanataka kuiboresha biashara ya t-shirt, wanahitaji kuanza kufikiria nje ya box kama wanavyofanya Weusi na wengine.

Njia nzuri ni kuwa na clothing line itakayokuwa na nguo za brand yako. Mfano mzuri brand ya Born 2 Shine ya B12 ilivyosimama. Imesimama kwasababu mtangazaji huyo wa Clouds FM ameamua kuconcentrate katika brand moja. Anachofanya ni kutofautisha tu designs za nguo anazotengeneza na kwa kufanya hivyo brand inazoeleka na inakuwa na nguvu sokoni.

Lakini kwa mtindo wa kutoa t-shirt leo zinaitwa ‘Mapenzi Matamu’, kesho ‘Mbona Umeniacha’ na kesho kutwa ‘Sikutaki Ondoka’, hakuna kitu cha maana msanii anaweza kunufaika zaidi ya fedha ndogo tu za kununua vocha na kulia bata za usiku mmoja.

Ni vyema kama wasanii wanapenda kufanya biashara ya t-shirt zenye majina ya single zao, basi zingekuwa zikitoka chini ya brand ama clothing line inayoeleweka. Kwa mfano naweza kuanzisha brand inaitwa ‘Pamba za Ukweli’ na nikawa natoa t-shirt zenye majina ya single zangu lakini ambazo zipo chini ya ‘Pamba za Ukweli’.

Maana yake ni kuwa ntakuwa natoa t-shirt au nguo za aina tofauti tofauti au zenye majina mbalimbali ya single zangu lakini ambazo zinaiimarisha brand ya ‘Pamba za Ukweli’.

Just a rondom a thought though.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents