Burudani

Rama Dee: Siungi mkono wasanii kuwekwa ndani kwa kutuhumiwa kujihusisha na unga

Muimbaji wa R&B nchini, Rama Dee, amedai kuwa haungi mkono zoezi linaloendeshwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwaweka baadhi ya wasanii ndani kwa kuwahusisha na madawa ya kulevya wakati wahusika wakubwa wanafahamika.

Kupitia mtandao wa Instagram, Rama Dee amefunguka kuwa angeuka mkono zoezi hilo endapo ingeweza kuzibwa njia ya ‘wauzaji papa’ ili kuwafikia wasanii na watu wote kwa ujumla.

Kupitia mtandao huo muimbaji huy ameandika:

Mimi kama msanii, Siungi mkono wasanii kuwekwa ndani Ila ninge muunga mkono Kama angeweza kuziba mirija ya Wauzaji Papa kuwafikia wasanii na watanzania kwa ujumla!
Toka nipo mdogo wauza unga wanafahamika na majina yao yapo kwenye mitandandao lakini sijawahi ona wakikamatwa wala kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari! Hata hao polisi pia sijaona picha zao!
Wasanii ni watu Kama watu wengine tu… so unapo anza kuaribu biashara zao kwa sababu tu upo na power ya uwongozi sidhani kama ni busara!

Ushauri wangu kaa na viongozi wenzio ambao walikutangulia kwenye uwongozi uliza why walishindwa then anzia hapo! Unajuwa haya mambo unaweza ona ya kawaida Ila yanaweza kuharibu maisha ya watu kuliko hata huwo Unga! Haswa wasanii.

Namuunga mkono Nape kuwa kuna njia za kutumia ambazo zinalinda sheria ya mtuhumiwa! Ila ukitumia nguvu bila Akili ni sehemu mojawapo ya kuwapatia pesa Wanasheria bila msingi wowote! Kukamata watu kwa kuhisi ni utaratibu mbaya sana! Kumbuka kuna watu wapo na chuki za maendeleo ya watu wengine.Unaweza ukasikia hata Tale anauza unga ambae ni rafiki yako, sijuwi utafanyaje hapo.
Mimi naona plan yako imeanzia sehemu si sahihi rudi nyuma Anza tena ni hayo tu, halafu hakuna movement nzuri Kama movement ya kutumia power ya wasaniii na jamii kiujumla. Fanya kazi yako Mh. makonda waache wasanii watafute mkate wao wa kila siku! Rama Dee!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents