Habari

Rama Dee ashangazwa na wasanii wanaoshindwa kuhoji kasoro za Kili Awards

Muimbaji wa R&B Rama Dee ambaye kwa muda mrefu alikuwa nchini Australia na familia yake, amesema ameshangazwa na jinsi wasanii wenzie walivyoshindwa kuitumia nafasi ya kwenye semina ya wasanii katika tuzo za Kili kwa kuuliza maswali ya msingi.

557945_597316006964573_460672922_n

Kupitia Twitter Rama ambaye wimbo wake pia umetajwa kuwania tuzo hizo amesema hiyo ni sababu moja ya kwanini wasanii hawaheshimiki.

“Shida ni yetu sisi wasanii Jana nimejifunza vitu vingi sana sioni Kama tunaweza kuheshimiwa #pumba,” ametweet.
“Wasanii wanafurahia Bia na bahasha kwenye Semina za Kilimanjaro hawachangii wala kuuliza maswali ya msingi wengine.”

“Nilipotoa maoni kwenye Semina ya Kilimanjaro THT iingie Kama Kikundi kwenye Kilimanjaro siku maanisha nipo na matatizo na wasanii wa THT.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents