Tragedy

Rais wa Venezuela Hugo Chavez afariki kwa kansa

Mamia ya wavenezuela walikusanyika mbele ya hospitali ambapo kiongozi wao Hugo Chavez alifariki jana kutokana na ugonjwa wa kansa.

Venezuelan President Hugo Chavez salutes during a military parade to commemorate the 20th anniversary of his failed coup attempt, on February 4, 2012, in Caracas.    AFP PHOTO/JUAN BARRETO

Miongoni mwao walionekana wakipepea bendera za Venezuela huku wengine wakiwa na mabango yenye maandishi, “People, Chavez and revolution, the battle continues”, na kusikika watamka “Chavez lives”. Rais huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 58.

Kutokana na kifo hicho, serikali imetenga siku saba za maombolezo ya kitaifa. Wananchi wengi wamekusanyika kwenye maeneo ya wazi kwenye mji mkuu Caracas na miji mingine wakiimba wimbo wa taufa, wakibubujikwa na machozi na kushika picha za kiongozi huyo.

“Asingefariki. Alikuwa rais bora kuwahi kutokea Venezuela,” alisema Frank Aponte, 45, aliyekuwa kwenye mtaa mmoja wa Caracas. Shughuli za kuuaga mwili huo mbele ya viongozi wengine wa kimataifa zitafanyika Ijumaa.

Katiba ya nchi hiyo inasema uchaguzi lazima ufanyike ndani ya siku 30 tangu kifo cha rais lakini serikali bado haijatangaza tarehe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents