Michezo

Rais wa shirikisho la tennis Urusi apigwa faini kwa kuwaita Serena & Venus ‘The Williams brothers’

Rais wa shirikisho la mchezo wa tennis nchini Urusi, Shamil Tarpischev amepigwa faini ya $25,000 kwa kuwaita Serena na Venus Williams “the Williams brothers” kwenye mahojiano ya TV.

Wimbledon-2008-Day-9-Venus-Williams-Serena-Wi_997441

Tarpischev pia alipigwa marufuku ya mwaka mzima kutojihusisha na ziara ya wanawake hao.

Mkurugenzi Mkuu wa chama cha tennis cha wanawake, Stacy Allaster alisema maneno hayo yanadhalilisha na hayana nafasi kwenye mchezo huo.

Rais wa chama cha tennis cha Marekani, Dave Haggerty amemtaka Tarpischev kuomba radhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents