Burudani

Rais wa shirikisho la Muziki, Addo November ajitosa ubunge wa bunge la Afrika Mashariki

Rais wa shirikisho la Muziki nchini, Addo November amejitosa kugombea nafasi ya ubunge wa bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambapo Ijumaa hii amerudisha fomu.

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii muda mchache baada ya kurudisha fomu katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba jijini Dar es salaam, Addo amedai kwa sasa anataka kuwatumikia watanzania kwa mapana zaidi.

“Shirikisho la Muziki kule ni kazi ambayo najitolea huku ambako nataka kwenda naenda kufanya kazi, kazi ya kitaifa zaidi katika wigo mzima wa Afrika Mashariki kuhakikisha tunatetea maslahi ya Watanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha kwamba interest za Watanzania tunazilinda,” alisema Addo.

Aliongeza, “Unajua Jumuiya iliyopita tulipoteza mambo mengi sana, tulipoteza ndege, tulipoteza pesa, tulipoteza rasilimali nyingi sana. Lakini wakati huu tutahakikisha Watanzania wananufaika fursa za Afrika Masharikui, kama hivi karibuni tulivyomuona Rais wetu Magufuli alivyowatafutia madaktari wetu 500 nafasi nchini Kenya na sisi tutakuwa sehemu ya kutatua changamoto za wananchi,”

Kuhusu nafasi yake ya Urais wa Shirikisho la Muziki nchini, Addo amedai kama akipata ataacha nafasi hiyo ichukuliwe na watu wengine wakati yeye akiendelea kuisaidia Tanzania kwa ujumla.

Zaidi wa watu 400 wanagombea nafasi 8 za kuiwakilisha Tanzania katika bunge hilo la Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents