Habari

Rais Mugabe aongoza list ya marais wenye umri mkubwa duniani, atimiza miaka 93

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe Jumanne hii anatimiza miaka 93 na kuwa rais mwenye umri mkubwa zaidi Duniani.

Alizaliwa mnamo mwaka 1924 pia aliwahi kufungwa jela mwaka 1964 na kutoka mwaka 1974 kwa kosa la kutoa hotuba ya kuihujumu Serikali.

Lakini pia Umoja wa Ulaya(EU) umemuongezea muda wa vikwazo Mugabe, yeye pamoja na Mkewe Grace kwa mwaka 1 hadi tarehe 20 Februari mwakani.

Hata hivyo Rais Mugabe amesema kuwa Donald Trump hakuwa chaguo lake upande urais wa Marekani lakini pia hakupenda

Bi. Clinton ashinde kwakuwa angekuja kusimamia na kuviendeleza vikwazo iliyopewa nchi ya Zimbabwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents