Michezo

Rais Malinzi atoa pongezi kwa timu ya Lipuli ya Iringa

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameuandikia barua uongozi wa timu ya Lipuli ya Iringa kwa mafanikio ya kupanda daraja msimu huu kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimuwa 2017/18.

????????????????????????????????????

Lipuli ya Iringa imepanda daraja baada ya kupita miaka 17 na Rais Malinzi amesema katika barua yake hiyo kwenda kwa Katibu Mkuu wa Lipuli, akisema: “Nitumie fursa hii kukupongeza wewe, uongozi wa klabuy ako, benchi la ufundi na wadau wote wa timu ya Lipuli kufuatia kupanda daraja kwenda Ligi Kuu.

“Bila shaka ni kazi kubwa imefanyika ikihusisha kujitolea kwa ari na mali kuhakikisha mnafika hapa mlipo,” ilisema barua hiyo na kuongeza: “Rai yangu kwenu ni kuongeza juhudi na kuendesha klabu kwa weledi mkubwa zaidi ili muweze kuwa washindani wa kweli katikal igi.”

Lipuli iliyo kuwa kundi “A” imepanda daraja na kuzipiku timu zaK iluvya United ya Pwani, Pamba ya Mwanza, African Sports yaTanga, Polisi Dar, Ashanti United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents