Habari

Rais Magufuli kwa CHADEMA: Andamaneni mkione cha mtema kuni

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaonya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliotangaza kuongoza maandamano kuanzia Septemba 1 mwaka huu.

b4444

Rais Magufuli ambaye alikabidhiwa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) siku sita zilizopita, ameanza ziara ya kufanya mikutano ya hadhara katika mikoa mbalimbali kama ilivyotarajiwa ambapo leo alikuwa mkoani Singida.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wilayani Manyoni, Singida Magufuli amenukuliwa akijibu tamko lililotolewa juzi na Chadema kwa kusema, hatua kali zitachukuliwa kwa viongozi hao wa Chadema.

“Wale wanaotangaza kufanya maandamano, watangulie wao wenyewe halafu watakiona cha mtema kuni. Mimi nataka watangulie wao wasiwatangulize watoto wa masikini,” amesema Rais Magufuli huku akiongeza kuwa;

“Wao wanakaa gesti (nyumba za kulala wageni) halafu wanawapa viroba watoto wa masikini ili watangulie kuandamana, sasa mimi nataka watangulie wao halafu waone.”

Julai 27 mwaka huu, Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe alitangaza kuwa chama hicho kitafanya mikutano ya hadhara na maandamano nchi nzima ili kupinga kile alichokiita udikteta wa serikali ya awamu ya tano.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents